Blackberry ni moja kati ya simu ambazo zilipata umaharufu mkubwa sana kabla ya kuja kwa Android na iOS, mambo yalibadilika sana kwa kampuni hiyo baada ya kuja kwa mifumo hiyo kiasi cha kulazimisha kampuni hiyo kubadilika na kuamua kutumia mfumo wa Android.
Hivi sasa baada ya kampuni hiyo kukabidhi swala zima la utengenezaji wa simu zake kwa kampuni ya TCL, Blackberry mercury ndio itakuwa simu ya kwanza kutengenezwa na kampuni hiyo baada ya uamuzi mzito wa kukabidhi utengenezaji wake kwa TCL. Blackberry itaendelea kutengeneza software pamoja na kueka ulinzi kwenye vifaa hivyo uku utengenezaji ukisimamiwa na TCL.
Blackberry Mercury sio jina rasmi bali jina la simu hiyo litaenda kujulikana huko nchini Barcelona kwenye mkutano wa MWC utakao fanyika tarehe 25 February mwaka huu ambapo ndio simu hiyo itazinduliwa rasmi. Hata hivyo simu hiyo ilitokea kwenye mkutano wa CES ambapo watu mbalimbali walifanikiwa kuiona pamoja na kuona muundo wake.
Hata hivyo muonekano huo bado haujakamilika kwa asilimia 100 kwani TCL inasema kuwa kuna baadhi ya vitu vinaweza kubadilika. Kuhusu sifa za simu hiyo kwa mujibu wa tovuti ya Android Authorty TCL walikataa kabisa kuweka wazi sifa za simu hiyo wakidai kuwa simu hiyo bado iko kwenye matengenezo hivyo hawako tayari kuweka wazi sifa za simu hiyo.