Mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Microsoft Bill Gates, hivi karibuni amatangaza kujitoa rasmi kwenye bodi ya uongozi wa kampuni hiyo. Bill Gates ambaye alianzisha kampuni ya Microsoft kama mwanzilishi mwenza, hapo siku ya jana tarehe 13 ametangaza hayo kupitia kwenye tovuti ya habari ya Microsoft.
Bill Gates alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo hadi mwaka 2000 alipo amua kuachia wazifa huo na kuendelea na harakati za kuendeleza foundation yake na mkewe inayo julikana kama Bill and Melinda Gates Foundation. Kwa mujibu wa tovuti ya Reuters, Mwaka 2008 Bill Gates aliamua kuachana na kazi zake za kila siku ndani ya kampuni ya Microsoft na kuamua kuangalia zaidi maswala ya uhisani.
Hata hivyo inaonekana Bill gates aliendelea kuwa mmoja wa viongozi kwenye bodi ya kampuni ya Microsoft hadi siku za karibuni alipo amua kujitoa kwenye bodi hiyo. Gates bado atatumika kama “mshauri wa teknolojia” kwa Mkurugenzi Mtendaji wa sasa Satya Nadella, jukumu ambalo alianza kulifanya mnamo 2014 kutokana na ombi la Nadella pale Bill Gates aliposhuka kutoka kwenye cheo cha mwenyekiti wa bodi ya Microsoft.
“Imekuwa heshima kubwa na fursa kubwa kufanya kazi na kujifunza kutoka kwa Bill kwa miaka yote. Bill alianzisha kampuni yetu kwa imani katika nguvu ya demokrasia ya programu na shauku ya kutatua changamoto kubwa za jamii. “Nadella alitoa maoni katika taarifa hiyo.
“Bodi imefaidika kutoka kwa uongozi na maono ya Bill. Na Microsoft itaendelea kufaidika na mawazo na ushauri wa kiufundi wa Bill unaoendelea kuendesha bidhaa na huduma zetu mbele. Ninashukuru kwa urafiki wa Bill na ninatazamia kuendelea kufanya kazi pamoja naye ili kufikia lengo letu la kumwezesha kila mtu na kila shirika duniani kufanikiwa zaidi. ” alisema sehemu ya taarifa hiyo ikiwa ni maneno ya mkurugenzi mtendaji wa sasa wa Microsoft Satya Nadella.
Bill Gates ameamua kuachia wazifa huo ili kuendelea na kazi yake ya uhisani ambayo hufanywa na foundation yake ya Bill and Melinda Gates Foundation.