Kama wewe ni mmoja wa watu ambao bado hawaja anza biashara yoyote mtandaoni basi pengine huu ni wakati wako. Kwa siku ya leo nitaenda kuelekeza kuhusu biashara ya mtandaoni ambayo nadhani watu wengi hawafahamu lakini inaweza kukusaidia kubadilisha maisha yako.
Biashara hii ni “Printing On Demand”, kupitia makala hii nitakueleza biashara hii inafanywaje ikiwa pamoja na njia rahisi ambazo unaweza kuzitumia kuanza biashara hii siku ya leo bure kabisa bila kutumia gharama yoyote
Najua una haraka kidogo ya kufahamu hivyo sita kupotezea muda wako hivyo moja kwa moja twende kwenye makala hii.
TABLE OF CONTENTS
Nini maana ya “Printing On Demand”
Printing on Demand ni biashara ambayo hufanya na watu wengi sana bila watu kujua kama biashara hii inafanya na watu gani..! Kwa kifupi “Printing On Demand” ni biashara ya kuuza nguo mtandaoni bila kuwa na duka mtandaoni bali wazo la muonekano wa nguo.
Jinsi biashara hii inavyofanya kazi ni kuwa, wewe unategengeneza logo au maandishi fulani ambayo ungependa yawe kwenye nguo fulani.
Kisha baada ya kutengeneza logo au maandishi hayo, kupitia kwenye tovuti za “Printing On Demand” utaweza ku-upload logo, maandishi au mchoro wako na kampuni hizo zitaweka mchoro huo kwenye bidhaa mbalimbali kama tisheti, makava ya simu na vitu mbalimbali na kuonyesha kwenye tovuti zao.
Pale mtu atakapo kuja na kununua moja ya bidhaa yenye mchoro wako, moja kwa moja kampuni hiyo hutuma mchoro wako kwa kampuni za ku-print na moja kwa moja mchoro wako utawekwa kwenye tisheti au bidhaa yoyote ambayo mteja kachagua na kisha kuituma kwa mteja aliye nunua.
Baada ya kampuni husika kutoa gharama zake za ku-print, usafirishaji na asilimia zao moja kwa moja hukupa kiasi kilicho bakia, na hivyo utaweza kupata sehemu ya asilimia ya mauzo yoyote yatakayo fanyika kupitia mchoro au logo yako.
Kifupi ni kwamba, mchoro wako utaweza ku-printiwa pale tu mteja atakapo kuwa ameweka oda ya kununua bidhaa husika ndio maana biashara hii inaitwa “Printing On Demand”.
Jinsi ya Kuanza Biashara Hii
Zipo njia nyingi za kuweza kuanza biashara hii kwa haraka na urahisi, lakini pia zipo njia ambazo ni maalum kwa watu ambao tayari wamesha fanikiwa na wana uwezo wa kutafuta masoko na washirika wa biashara. Lakini leo ngoja tuongelee njia rahisi za kuanza biashara hii.
Kwa ufupi biashara hii ina faida nje ya nchi na sio kwa watanzania, hivyo wakati unafikiria kuanza biashara hii fikiria kuangalia zaidi wateja wa nje ya Tanzania.
Kwa sasa zipo tovuti nyingi zinazo ruhusu mteja kuuza bidhaa kwa njia ya “Printing On Demand”, lakini ni tovuti chache sana zinazo ruhusu nchi zote kuuza bidhaa kwa njia hii. Kuliona hilo nimekuletea tovuti hii moja ambayo inaruhusu wewe kuuza bidhaa kwa njia hii.
Kufahamu zaidi angalia video hii hapa chini kwa kufuata hatua kwa hatua, angalia biashara ya kwanza kuweza kujua jinsi ya kuanza biashara hii.
Kitu cha muhimu hakikisha una tengeneza akaunti kupitia tovuti hiyo kupitia link hapo chini kisha moja kwa moja anza kuweka picha zako na moja kwa moja utaweza kuanza kutengeneza pesa mtandaoni kupitia njia hii ya “Printing On Demand” kupitia tovuti hii.
Kama unataka kuangalia mfano wa bidhaa ambayo binafsi nimefanikiwa kuuza kwenye mtandao huo unaweza kuangalia kwenye picha hapo chini.
Njia hii ni bora sana na inaweza kukusaidia kupata pesa mtandaoni kwa haraka hivyo hakikisha unaifanya kwa usahihi kwani wapo watu wanatengeneza mamilioni ya pesa kwa kutumia njia hii. Unaweza kuangalia video hapo chini na il kuamini kuhusu njia hii.
Video ni nyingi sana guys unaweza kuingia YouTube na kutafuta mwenyewe kuhusu biashara hii na uhakika utaweza kujifunza mengi.
Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kuanza biashara ya dropshipping kama unahitaji kufanya biashara hii.