Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Zifahamu Hizi Hapa Aina 5 za Biashara Zinazolipa Zaidi Mtandaoni

Biashara hizi pia zinakuja na changamoto zake hivyo ni vizuri kuchagua unayoiweza
Zifahamu Hizi Hapa Aina 5 za Biashara Zinazolipa Zaidi Mtandaoni Zifahamu Hizi Hapa Aina 5 za Biashara Zinazolipa Zaidi Mtandaoni

Linapokuja swala la biashara mtandaoni ni wazi kuwa kila mtu ana upeo wake pamoja na uzoefu unaomsaidia kupata pesa mtandaoni, lakini pia kufanya biashara mtandaoni hasa ukiwa Tanzania unahitaji kuangalia aina fulani za biashara ambazo hizo pengine zinaweza kukusaidia zaidi kupata pesa mtandaoni hasa ukiwa afrika na Tanzania kwa ujumla.

Kupitia makala hii nitaenda kukujuza aina tano za biashara ambazo zinalipa zaidi mtandaoni hasa kwa hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla, kutu cha msingi ni kuwa na uvumilivu kusoma makala hii hadi mwisho na uhakika utapa mambo kadhaa ya kujifunza.

Advertisement

Kumbuka aina hizi za biashara zimechaguliwa kutokana na udogo wake wa mtaji, huku tukiwa na fikra kuwa wote tunataka kuanzia chini. Hivyo basi unaweza kuanza biashara hizi wakati wowote kitu cha msingi ni uvumilivu na adabu ya kufanya mambo hayo kwa umakini.

5. Anzisha Tovuti au Blog

Ukweli ni kwamba, Google bado inauhitaji wa tovuti hasa tovuti za kiswahili. Lakini hapa sina maana kuwa na tovuti ni tovuti hapana, bali hapa nina maana tovuti zenye kuleta maana na kutoa mchango wa thamani kwa wasomaji kila siku na sio kuangazia maswala ya kipato pekee. Lakini wazo hili la biashara mtandaoni limekuwa ni la mwisho kwa sababu kuwa na tovuti pekee sio chanzo cha mapato bali unahitaji kuwa na vyanzo vya ziada kuweza kuhakiksha tovuti hiyo inakuingizia faida.

4. Anzisha YouTube Channel

Sambamba na kuanzisha tovuti unaweza pia uka anzisha YouTube channel lakini ni muhimu kuwa na picha pana ya unapokwenda kwani watu wengi wamekuwa wakianzisha channel bila kuwa na muelekeo wakiwaza kwamba unaweza kuwa tajiri kwa haraka kwa kuchapisha habari au video zisizokuwa na maana. Ukweli ni kwamba kuwa na channel hasa hapa Tanzania unahitaji kutengeneza ubora wa video zako pamoja na mada zako ziwe na mchango lakini pia unatakiwa kujua unapokwenda kwani asikudanganye mtu yoyote matangazo ya Google Pekee hayatoshi.

3. Kutafuta Masoko Kwa Niaba ya Makampuni (Affiliate Marketing)

Ukweli ni kwamba hakuna kampuni ambayo haina kitengo cha kutafuta masoko, kama kwa namna yoyote umefanikiwa kutengeneza jina mtandaoni au unaweza kutoa ushawishi mtandaoni basi unaweza kufanya biashara ya affilate marketing. Lakini kama zilivyo biashara nyingine kwenye listi hii pia nayo hii inakuja na changamoto zake. Kama unafanya kazi hii kwa hapa Tanzania ni lazima kuwa na jina kubwa sana ndipo uweze kufanikiwa kwani watu wanahitaji mtu muaminifu na uaminifu hauji kwa maneno bali kazi na muda mrefu wa kujituma bila kuwaza faida.

Vilevile kama unafanya kazi hii na kampuni za nje ya Tanzania bado kuna changamoto kubwa sana ya njia za malipo hasa kwa wanunuaji pamoja na njia za kuweza kupokea fedha zako baada ya kutengeneza faida.

2. Ushawishi Kwenye Mitandao ya Kijamii (Social media influencer)

Kwa sasa kama umekuwa ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii hasa Instagram lazima unajua kuwa kuna baadhi ya watu wanafanya matangazo ya makampuni fulani kupitia akaunti zao hii ndio inaitwa social media influencer, hapa sisemi matangazo ya vipodozi au matangazo madogo madogo bali mara nyingi watu hawa hupewa bidhaa na makampuni makubwa kuweza kujaribu au kutumia na baadae kutangaza kwenye akaunti zao za mitandao ya kijamii. Lakini biashara hii kama zilivyo biashara nyingine nayo pia inakuja na changamoto.

Ili kuweza kufanya biashara hii unahitaji kuwa na wafuasi wengi na pia unahitaji kuhakikisha wewe mwenyewe unajiweka kwenye mazingira bora ya kushawishi kampuni kuweza kufanya kazi na wewe, akaunti yako isiwe yenye kuvunja sheria za nchi au kukiuka maadili kwa namna moja amba nyingine lakini kikubwa kabisa unatakiwa kuwa na ushawishi mkubwa kupitia mitandao yako hiyo.

1. Kuwanunulia Wateja Bidhaa Kutoka Mtandaoni (Drop shipping)

Kama wewe ni mpenzi wa biashara mtandaon basi lazima utakuwa kwa namna moja ama nyingine umeshawahi kuwaza kununua kitu kutoka mtandaoni, lakini kutokana na sababu kama njia rahisi za malipo pamoja na njia za kufanya mzigo kukufikia kwa urahisi basi unakuta hatua hii ya kununua kitu inakuwa ni ngumu sana.

Ndio maana biashara ya kununulia watu vitu kutoka mtandaoni ni moja ya biashara bora sana kwa sasa hapa Tanzania. Biashara hii inahusisha kununua bidhaa kwenye tovuti kubwa kama vile Amazon, Ebay na nyingine kama hizo na kusafirisha bidhaa hizo moja kwa moja kwa mteja bila mteja kuwa na mawasiliano na kampuni husika, mteja hukulipa wewe kiasi fulani cha pesa ambacho hichi hutosha kulipia gharama zote pamoja na wewe kupata faida kwa kiasi fulani.

Mara tu mzigo unapofika mteja huja kuchukua kwenye ofisi zako au huletewa na kampuni za usafirishaji ambazo unakuwa unafanya nazo kazi, uzuri wa biashara hii unaweza kufanya bila hata ya kuwa na ofisi lakini unahitaji kuwa na uaminifu mkubwa ambao huu unapatikana kwa kuwa na jina kubwa pamoja na kufanya biashara hiyo kwa muda mrefu kidogo.

Na hizo ndio baadhi ya biashara ambazo ukweli unaweza kufanya na kuona faida hasa ukiwa hapa Tanzania. Kitu cha msingi unatakiwa kujua kuwa kila biashara inakuja na changamoto zake na pia kila biashara inahitaji uvumilivu pamoja na adabu ya kuendelea kufanya kila siku bila kutegemea faida kubwa hasa pale unapokuwa una anza. Kama unataka kujua zaidi soma hapa kujua mambo ya msingi ya kuzingatia kabla ya kuanza biashara yoyote mtandaoni.

Mtu yoyote asikukatishe tamaa, jambo lolote ukilifanya kwa umakini na ustadi litafanikiwa siku moja, usikate tamaa.

8 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use