Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Simu Mpya, iPad Pro (2021), Tecno Spark 7, Infinix Hot 10S

Hizi hapa simu mpya zilizotoka wiki hii..
Simu Mpya, iPad Pro (2021), Tecno Spark 7, Infinix Hot 10S Simu Mpya, iPad Pro (2021), Tecno Spark 7, Infinix Hot 10S

Wakati tukiwa bado tupo mwezi mtukufu wa ramadhani, kwa upande wa teknolojia napo mwezi huu huwa mwezi ambao upo bize sana kwa kampuni mbalimbali zinazo tengeneza simu.

Kama wewe ni msomaji wa tovuti ya Tanzania tech basi najua kuwa unajua tuna kipengele maalum cha simu mpya na hapo unaweza kujua simu zote mpya zilizotoka kila mwezi, lakini kutokana na watu wengi kutokujua sehemu hiyo sasa tutakuwa tuna walatea list ya nzima ya simu mpya kila wiki.

Advertisement

Kwa kuanza leo tumewaletea list ya simu mpya zilizotoka kipindi hichi ambapo kampuni ya Infinix hapo jana imetangaza simu zake mpya za Infinix Hot 10S na Infinix Hot 10s NFC ambazo ni bora sana kwa upande wa game na chaji.

Pia kampuni ya Apple nayo imetangaza bidhaa zake mpya ikiwa pamoja na iPad Pro 12.9 (2021), bila kusahau kompyuta yake mpya ya iMac ya mwaka (2021). Kwa watumiaji wa Appe pengine iPad Pro (2021) ni iPad yenye mabadiliko makubwa kuliko iPad zote hivyo ni muhimu kusoma zaidi kuhusu hii.

Mbali na hayo kampuni ya Tecno pia imezindua simu mpya za Tecno Spark 7, na Tecno Spark 7p ambazo pia zimezinduliwa hapa Tanzania zikiwa na sifa tofauti na zile za India, kwa sasa bado tunafuatilia ili kupata sifa kamili pamoja na bei za simu hizi za Spark 7 za hapa Tanzania.

Kwa sasa huwezi kununua Spark 7 hadi itakapofika mwanzoni mwa mwezi wa Tano, natumaini hadi hapo tutakuwa tumeshajua sifa pamoja na bei rasmi ya simu hizi mpya kutoka Tecno.

Pia mbali na hayo, kwa mujibu wa tovuti ya GSMArena inasemekana kuwa kampuni ya Tecno inatarajia kuingiaza sokoni simu mpya ya Tecno Camon 17 ambayo kwa sasa tayari imesha jitokeza kwenye baadhi ya tovuti huko nchini Kenya, unaweza kuona picha halisi ya simu hiyo hapo chini.

Simu Mpya, iPad Pro (2021), Tecno Spark 7, Infinix Hot 10S

Hayo na mengine mengi unaweza kuangalia list nzima kwa kubofya hapo chini, na utapelekwa kwenye sehemu maalum ya kujua sifa pamoja na bei za simu hizi mpya kwa hapa Tanzania.

Soma Hapa Kujua Simu Mpya

Kama unataka kuendelea kujua zaidi kuhusu simu mpya, laptop mpya na smartwatch mpya basi hakikisha unatembelea tovuti ya Tanzania tech kila siku. Kwa habari zaidi za teknolojia na maujanja pia endelea kutembelea Tanzania tech.

3 comments
  1. Nimeshindwa kupata baadhi ya simu mnazozitangaza na pia mnatoa bei jambo zuri lakini mngekuwa mnatoa na maeneo zinakopatikana mngetusaidia sana maana wengine tunapigwa kwa kusumbuka kuzitafuta

  2. Samahani wakuu hi simu ya infinix hot 10s naweza ipata wapi maana nimeulizia sana lakini lakini majibu oo hakuna simu Kama hiyo

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use