Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Infinix Yazindua laptop yake ya Kwanza Inbook X1 na X1 Pro

Kampuni ya Infinix yaingia rasmi kwenye biashara ya laptop, yazindua laptop ya kwanza
Infinix Yazindua laptop yake ya Kwanza Inbook X1 na X1 Pro Infinix Yazindua laptop yake ya Kwanza Inbook X1 na X1 Pro

Kampuni ya Infinix imekuwa ikijulikana sana kwa utengenezaji wa simu janja zenye sifa nzuri na ambazo huuzwa kwa bei nafuu, mbali na hayo kampuni hii ambayo ni ndugu na kampuni ya TECNO zote zimekuwa zikifanya vizuri sana hasa hapa Afrika kwa uuzaji wa smartphone.

Kuongeza wigo mkubwa zaidi kwa wateja wake, Mara baada ya kuingia kwenye biashara ya TV, hivi karibuni kampuni ya Infinix imeongeza upana wa bidhaa zake kwa kuingia rasmi kwenye biashara ya laptop.

Advertisement

Kampuni ya Infinix imeingia rasmi kwenye biashara hiyo ya laptop kwa kuzindua laptop yake ya kwanza ya Inbook X1 (2021). Laptop hii inakuja na sifa nzuri na pia tayari inapatikana kwa baadhi ya nchi hapa Afrika.

Sifa za Inbook X1

Infinix Inbook X1 inakuja na processor za Intel Core i3-1005G1, Core i5-1035G1 na Core i7-1065G7 kwa toleo la Inbook X1 Pro. Kwa upande wa RAM Inbook X1 inakuja na RAM za kuchagua kati ya GB 8 na GB 16, kwa upande wa uhifadhi infinix Inbook X1 inakuja na SSD ya kati ya GB 256 na GB 512 zote zikiwa zimetengenezwa kwa teknolojia ya PCIe SSD.

Kwa upande wa muundo laptop hii imetengenezwa kwa aluminium huku ikiwa na kioo cha inch 14.0 ambacho kime tengenezwa kwa teknolojia ya FHD, kioo hichi kinaweza kujikunja kwa nyuzi 180 huku kwa juu kikiwa na kamera ya webcam 720p HD camera.

Infinix Yazindua laptop yake ya Kwanza Inbook X1 na X1 Pro

Mbali na hayo laptop hii pia inakuja na keyboard ya aina ya Backlit Chiclet Keyboard, ambayo iko flat kabisa.

Laptop hii pia inakuja na teknolojia ya DTS audio processing, Wi-Fi 6, Bluetooth 5.1 kwa toleo la kawaida na Bluetooth 5.2 kwa toleo la Inbook X1 Pro.

Laptop hii inakuja na port moja ya USB-C, sehemu mbili za USB 3.0 ports na sehemu moja ya USB 2.0 port, vile vile Inbook X1 na X1 Pro zinakuja na sehemu moja ya HDMI port, sehemu moja ya SD card slot, na sehemu moja ya kuchomeka headphone maarufu kama 3.5mm headphone na microphone jack.

Infinix Yazindua laptop yake ya Kwanza Inbook X1 na X1 Pro

Kuendesha laptop hii Inbook X1 inakuja na battery ya 55Wh ambayo ina support chaja ya 65W (USB-C) PD3.0 AC adapter. Infinix inadai kuwa laptop hii inauwezo wa kudumu na chaji masaa 11.

Moja kati ya sehemu mpya kwenye laptop hii ni pamoja na sehemu ya In-Sync, ambayo inakupa nafasi ya kuunganisha laptop hiyo na kutuma mafaili kati ya laptop hiyo na TV za Infinix, pamoja na smartphone za Infinix.

Infinix Yazindua laptop yake ya Kwanza Inbook X1 na X1 Pro

Kwa upande wa rangi Inbook X1 inakuja na rangi za Noble Red, Elves Green, Starfall Grey na Elegant Black.

Bei ya Inbook X1 na Upatikanaji

Kwa upande wa bei, laptop ya Infinix Inbook X1 inategemea kuanza kupatikana kuanzia mwezi ujao na itapatikana kwanza kwa nchi za Egypt, Indonesia, na Nigeria. Kwa upande wa bei unaweza kusoma hapa kujua bei ya laptop hii kwa hapa Tanzania.

Kama unataka kujua zaidi kuhusu laptop hii pindi itakapo fika hapa Tanzania hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use