Bei na Sifa za ViVo X21 UD Simu Yenye Fingerprint Kwenye Kioo

Hatimaye sasa utaweza kufungua simu yako kwa kutumia fingerprint kwenye kioo
Bei na Sifa za ViVo X21 UD Simu Yenye Fingerprint Kwenye Kioo Bei na Sifa za ViVo X21 UD Simu Yenye Fingerprint Kwenye Kioo

Baada ya kutangazwa rasmi kupitia mkutano wa CES 2018, Hatimaye simu ya kwanza yenye ulinzi wa fingerprint kwenye kioo, ViVo X21 UD imetangazwa kutoka siku ya leo huko nchini india, Simu hii ina andika rekodi kwa kuwa simu ya kwanza kabisa kuwa na uwezo wa fingerprint juu ya kioo.

Mbali na hayo simu hii ni toleo la pili la simu ya Vivo X21 ambayo yenyewe ilikuwa na fingerpirt kwa nyuma, lakini toleo hili la simu hii ya sasa ya ViVo X21 UD yenyewe ndio itakuwa simu ya kwanza yenye sehemu ya ulinzi ya fingerprint juu ya kioo.

Advertisement

Kwa upande wa sifa simu hii haina tofauti sana na toleo la kwanza la simu hii la Vivo X21 ambayo yenyewe ilizinduliwa rasmi mwezi wa tatu na ilikuwa maalum kwa nchi za China. Sifa za simu hii ya Vivo X21 UD ni kama zifuatazo.

Sifa za Vivo X21 UD

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.28 chenye teknolojia ya Super AMOLED display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 11080 x 2280 pixels, 19:9 ratio (~402 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.2 GHz Kryo 260 & 4×1.8 GHz Kryo 260), Qualcomm SDM660 Snapdragon 660 Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 512
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
  • Ukubwa wa RAM – GB 6
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 12, yenye f/2.0, 1080p.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye uwezo wa (f/1.8, 1/2.5″, 1.4µm, Dual Pixel PDAF) na nyingine ikiwa na Megapixel 5 yenye (f/2.4), huku zote zikiwa na uwezo wa phase detection autofocus, LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3200 mAh battery yenye teknolojia ya (Fast battery charging).
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS, 3.1, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Black na Ruby Red.
  • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint Kwenye Kioo (Kwa Mbele).

Bei ya Vivo X21 UD

Kwa upande wa bei ya simu hii ya Vivo X21 UD, simu hii inakuja ikiwa inauzwa kwa Rupia ya india ₹35,990 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 1, 211,000. Kumbuka bei hii inaweza kubadilika kwa hapa Tanzania kwa sababu ya kodi na kupanda kwa viwango vya kubadilisha fedha.

Unaweza kununua simu hii kupitia soko la mtandaoni la india la flipkart, unaweza kuangalia simu hiyo kwenye soko hilo Hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use