Baada ya kusubiria kwa muda mrefu hatimae kampuni ya Tecno imezindua simu mpya ya Tecno Spark 2, simu hii kama tulivyo ona kwenye tetesi inakuja na sifa nzuri kwa matumizi ya kila siku pamoja na muonekano huku ikiwa na kioo kikubwa cha Full Display.
Hapa tutaenda kuangalia sifa za Tecno Spark 2, pamoja na kujua makadirio ya bei ya simu hii kwa hapa Tanzania. Simu hii inaendeshwa na processor ya MediaTek MT6580WP chip yenye Quad-Core processor na mfumo wa 64-bit CPU. Vilevile Tecno Spark 2 inakuja na processor yenye uwezo wa Cores nne 4 ambazo zina wezesha speed ya 1.4GHz. Kuwezesha game kufaya kazi kwa urahisi Tecno Spark 2 inakuja na GPU ya ARM Mali-400 MP2 graphics card yenye speed ya 416MHz. Tecno Spark 2 inatumia mfumo wa Android Go Oreo, mfumo ambao unafanya simu hii kuwa na RAM ya GB 1. Sifa nyingine za Tecno Spark 2 ni kama zifuatazo.
Sifa za Tecno Spark 2
- Ukubwa wa Kioo – Inch 6.00 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na 720 x 1440 pixels, 18:9 ratio (~274 ppi density)
- Mfumo wa Uendeshaji – Android GO 8.1 (Oreo)
- Uwezo wa Processor – quad-core 1.3 GHz ARM Cortex-A7 MediaTek Mt6580 chipset
- Uwezo wa GPU – Mali-400MP2
- Ukubwa wa Ndani – GB 16 ikiwa na uwezo wa kuongezewa kwa Memory card hadi ya GB 128.
- Ukubwa wa RAM – GB 1
- Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8 MP, f/2.4 dual-LED flash.
- Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 13 autofocus, quad-LED flash
- Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3500 mAh battery
- Viunganishi – Wi-Fi 802.11 b/g/n, Bluetooth v4.2, A2DP, LE
pamoja na GPS ya A-GPS, microUSB 2.0 - Rangi – Inakuja kwa rangi za Champagne Gold, Choral Blue, Metal Silver and Phantom Black
- Mengineyo – Inayo Line Mbili za Dual SIM
- Ulinzi – Fingerprint (iko nyuma), Face Unlock (kufungua simu kwa uso)
- Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
Simu ya Tecno Spark 2 inakuja na kava la plastiki ndani ya box ambalo linakusaidia kuweza kulinda simu yako isiharibiwe na mikwaruzo, mbali na hayo simu hii inakuja na headphone, chaji na kadi ya warrant pamoja na kadi ya Boom Play. Tecno Spark 2 ni simu ya bei nafuu kwa ajili ya wapenzi wa simu za tecno.
Bei ya Tecno Spark 2
Kwa upande wa bei ya Tecno Spark 2, simu hii inakuja kwa makadirio ya bei ya kawaida ya Tsh 300,000 hadi Tsh 350,000. Kumbuka bei inaweza kubadilika, Tecno Spark 2 inategemewa kuanza kupatikana hivi karibuni kupitia maduka ya Tecno pamoja na kwenye soko la mtandaoni la Jumia.
Simu hi Haina uwezo wa kukonect na pc nlijarib kuhamisha baadh ya picha kutoka kwenye PC na iligoma
Nimezkubar sana hiz sim
Natafuta kioo Cha cm. Cm yangu imepasuka kioo baada ya kuanguka. Ni cm aina ya tecno spark 2.
Nauliza vioovyake zinapatikana Mimi kio kimepasuka
Maoni*jaman mm nataka kujua kati ya k9 na spark2 ipi kubwa?
Ivii kwa Nini cm zenu huwaa Zina stakii me apa natumia TECNO spak2 KA7 lakini inastakii mpakaa kerooo
Mm natumia Tecno spark 2 KA7 inazingua kushika H+ au 3G maeneo ambayo infinx zinashika. Nikitumia line ya vda naomb msaada nanna ya kuset
hv Tecno mbn mnatuchosh wateja wenu mtandao unapanda na kushuk Tena mnamwingne hady hnakela
Maoni* ongezen uyundu
Jamani ongezeni kasi kwenye mtandao upo chini sana
Bei ya screen complete ya spark2 samahan
Simu iko vizuri
mbona me natumia tecno spack 2 kwenye mtandao inaonesha 2G bax aisomi 3g wala 4G nifanyaje ili ikubali kusoma
kwa upande wangu hii simu aina ya tecno spark 2 haina tatizo kabisa katika kila vipengele, nahisi simu hizi zitakuwa na matoleo tofauti ndo maana wengine zinaonekana zinawasumbua