Hakuna shaka kuwa kwa sasa programu bora zaidi ya ujumbe wa papo hapo ni programu ya WhatsApp. Programu hii inakuja na sehemu bora mbalimbali ambazo zinaweza kusaidia kuwasiliana na uwapendao kwa urahisi na haraka.
Moja ya sifa muhimu za WhatsApp ni ujumbe wa sauti au WhatsApp Voice. Sehemu hii inaruhusu watumiaji kutumia ujumbe wa sauti kwa urahisi na haraka.
Lakini, kuna nyakati ambazo tunataka tu kubadilisha ujumbe huo wa sauti kuwa maandishi. Sababu inaweza kuwa kitu chochote, inaweza kuwa unalo tatizo la masikio au tatizo lingine kama hilo ambalo linakuzuia kusikiliza ujumbe huo.
Kupitia makala hii nitakuonyesha njia rahisi ya kubadilisha ujumbe wa sauti wa WhatsApp (WhatsApp Voice) kwenda kwenye ujumbe wa maandishi, bila kujali lugha iliyo zungumzwa. Basi bila kupoteza muda twende kwenye makala hii.
Badilisha Ujumbe wa Sauti Kuwa Maandishi
Hatua ya kwanza hakikisha unayo internet kwenye simu yako, kisha ingia kwenye soko la Play Store na kisha download app ya Live Transcribe kwenye simu yako. Unaweza kudownload app hii kwa kutumia link hapa, au unaweza kudownload kupitia link hapo chini.
Kubadilisha Lugha
Baada ya kudownload app hii washa app hii kisha ruhusu app hii kuweza kuhifadhi data kwenye simu yako kisha utaweza kuona screen kama hiyo hapo chini.
Baada ya kuona screen hapo juu sasa unaweza kuendelea kwenye hatua ya kuchagua lugha, kama unataka kubadilisha sauti ya kiingereza kuwa maneno ya kiingereza basi unaweza kuendelea kwenye hatua za chini yake. Kama unataka kubadilisha lugha kuwa Kiswahili au lunga yoyote basi fuata hatua hizi.
Bofya kitufe cha settings kilichopo chini kwenye kona upande wa wa kushoto, kisha unaweza kuangalia sehemu iliyoandikwa More Settings kisha Primary Language bofya hapo na chagua lugha ya Swahili.
Baada ya hapo sasa utaweza kuona kioo hicho hapo chini na kuona kioo hicho basi moja kwa moja utakuwa huko tayari kubadilisha meseji za WhatsApp za sauti kuwa ujumbe wa maneno.
Baada ya hapo sasa fungua WhatsApp kisha download meseji ya sauti unayotaka kubadilisha iwe maandishi kisha moja kwa moja play sauti hiyo kisha kwa haraka fungua app ya Live Transribe na moja kwa moja utaweza kuanza kuona maandishi yanayo zingumzwa kwenye meseji hiyo.
Kama unavyoweza kuona njia hii inafanya kazi vizuri sana hata kama upo kwenye sehemu yenye kelele kiasi, pia ni muhimu kujua kuwa mara baada ya app kusikiliza inaweza kubadilisha maneno ili kuwa na usahihi. Meseji hapo juu nilichukua screenshot haraka kabla haijamaliza kufanya mabadiliko na kuweka usahihi kwenye sentensi husika.
Njia Nyingine
Kama unataka kujaribu njia nyingine unaweza kujaribu njia zifuatazo ambazo hizi zinafaa kama mtu unataka kubadilisha ujumbe wa sauti wa kingereza kuwa ujumbe wa maandishi. Njia hizi ni rahisi na haraka.
Download App ya Transcriber for WhatsApp, unaweza kuipata hapa au unaweza kudownload kupitia hapo chini.
Baada ya ku-install app hii nenda kwenye ujumbe wa WhatsApp ambao unataka kubadilisha kisha moja kwa moja shikilia ujumbe huo na sehemu ya kushare itatokea kwa juu kisha bofya hapo na kisha chagua app ya Transcriber na moja kwa moja utaweza kuona ujumbe huo ukiandikwa kwa maandishi.
Baada ya hapo utaweza kuona maneno naliyo ongewa kwenye ujumbe wa sauti yakiwa juu ya kioo cha simu yako kama inavyoweza kuonekana kwenye picha hapo chini.
Baada ya hapo natumaini utakuwa umeweza kubadilisha ujumbe wa sauti wa WhatsApp kuwa ujumbe wa maandishi. Kama kuna sehemu yoyote umekwama unaweza kuuliza kupitia kwenye sehemu ya maoni hapo chini.
Kujifunza zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku kwani sasa tutakuwa tunapakia makala nyingi zaidi za kujifunza vitu mbalimbali. Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kutengeneza tovuti kama Twitter ndani ya dakika 10.