Instagram imekuwa ikibadilisha vitu mbalimbali kwenye app yake bila watu wengi sana kuweza kujua. Kwa siku ya leo nimekuletea moja ya sehemu hiyo ambayo inaweza kusaidia kubadilisha theme au muonekano kwenye sehemu ya DM kupitia app yako ya Instagram.
Kama unavyoweza kuona picha hapo juu, sehemu yako ya DM inaweza kuwa na muonekano mbalimbali kwa kuchagua theme mbalimbali kupitia njia hii nitakayo kuonyesha kupitia makala hii.
Kwa kuanza hakikisha una update app ya Instagram kupitia Play Store au App Store kisha baada ya hapo hakikisha una unganisha Instagram DM na Facebook Messenger, unaweza kufanya hivyo kwa kufuata hatua hapo chini.
Kuunganisha Instagram DM na FB Messenger
Ingia kwenye profile yako kwa kubofya alama ya mtu upande wa kulia chini.
Baada ya hapo bofya Menu ya mishale mitatu inayotokea juu upande wa kulia.
Baada ya hapo moja kwa moja chagua Settings.
Baada ya hapo chagua sehemu ya “Update Messaging”
Baada ya hapo chagua kitufe cha update.
Kwa kufanya hatua hizi utaweza kuanza kupokea meseji zako za Instagram DM pamoja na meseji za Facebook moja kwa moja kupitia profile yako ya Instagram au ya Facebook Messenger. Kumbuka baada ya kufanya hatua hii hutoweza tena kuachanisha DM na FB Messenger.
Kubadilisha Theme Kwenye Instagram DM
Baada ya kufanya hatua hizi rudi moja kwa moja kwenye ukurasa wa mwanzo kwenye app yako ya Instagram kisha moja kwa moja utaweza kuona alama ya messenger kwenye sehemu ambayo ilikuwa DM.
Bofya hapo moja kwa moja ili kuanza hatua za kubadilisha muonekano wa chat zako kupitia Instagram DM.
Kupitia ukurasa wako wa DM chagua chat ya mtu yoyote ambaye unataka chat yake iwe tofauti na nyingine kwa muonekano kisha bofya kitufe cha info kilichopo pembeni ya jina la mtu.
Baada ya hapo utaweza kuona sehemu ya Theme kwenye ukurasa huo.
Chagua sehemu hiyo na badilisha kulingana na mahitaji yako. Unaweza kuchagua theme ambazo tayari zimepewa majina, au unaweza kuchagua kulingana na rangi.
Kwa kufanya hatua hapo juu utaweza kubadilisha muonekano wa sehemu ya DM kupitia app ya Instagram na utaweza pia kuunganisha Instagram DM pamoja na Facebook Messenger.
Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa jinsi ya kutuma meseji zinazojifuta zenyewe kupitia mtandao wa WhatsApp. Kwa maujanja zaidi hakikisha una tembelea Tanzania tech kila siku.