Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Badili Mwandiko wa Kompyuta Kuwa Mwandiko wa Mkono

Utaweza kufanya mwandiko wa kompyuta kuwa mwandiko wa mkono
Badili Mwandiko wa Kompyuta Kuwa Mwandiko wa Mkono Badili Mwandiko wa Kompyuta Kuwa Mwandiko wa Mkono

Ni wazi kuwa ni rahisi sana kubadilisha mwandiko wa mkono au mwandiko ulio andikwa kwa mkono kuwa mwandiko ulio andikwa na kompyuta, lakini je ulishawahi kujiuliza unawezaje kubadili mwandiko ulio andikwa na kompyuta kuwa kama mwandiko ulioandikwa kwa mkono..?

Kama ulikuwa unajiuliza sana basi majibu yapo kwenye makala hii. Kupitia makala hii nitakuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kubadilisha mwandiko wa kompyuta kuwa mwandiko wa mkono.

Advertisement

Badili Mwandiko wa Kompyuta Kuwa Mwandiko wa Mkono

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, hayo ni maandishi ambayo yameandikwa kwa kompyuta na kubadilshwa kuwa maandishi yaliyo andikwa kwa mkono. Mbali na maandishi pia utaweza kuweka maandishi hayo kwenye mistari kama ilivyo kwenye daftari kama unavyo ona kwenye picha hapo juu.

Basi bila kuendelea kupoteza muda mwingi moja kwa moja twende kwenye hatua hizi muhimu. Kwa kuanza download app kupitia link hapo chini.

Download App Hapa

Baada ya kudownload unaweza kuzima data kwenye simu yako moja kwa moja kisha ndio ufungue app hii, hiyo inasaidia kwa kuwa app hii ina matangazo mengi sana lakini pia inaweza kufanya kazi bila Internet.

Baada ya kufungua app hii bofya sehemu ya Create New iliyopo chini upande wa kulia

Badili Mwandiko wa Kompyuta Kuwa Mwandiko wa Mkono

Baada ya hapo utaletewa ukurasa mpya kisha bofya kwenye ukurasa huo kufungua.

Badili Mwandiko wa Kompyuta Kuwa Mwandiko wa Mkono

Baada ya hapo utaletewa ukurasa mpya ambao unaweza kutumia kuandika maandishi yalio andikwa kwenye kompyuta na kuyabadilisha kuwa mwandiko ulio andikwa na mkono.

Badili Mwandiko wa Kompyuta Kuwa Mwandiko wa Mkono

Kwenye ukurasa huu unaweza kupaste maandishi yoyote ambayo ume copy kutoka sehemu yoyote hii ni rahisi kwa mwanafunzi au mtu yoyote ambaye anataka kuandika maandishi kwa haraka kutoka kwenye mfumo wa kuchapisha kuja kwenye mfumo wa mwandiko wa mkono.

Kwa kufanya hivyo natumaini utakuwa umeweza kubadilisha mwandiko wa kompyuta kuwa mwandiko wa mkono. Njia hii ni bora na inaweza kusaidia sana wanafunzi hasa pale ambapo unataka kuandika assgment ambayo ni lazima iandikwe kwa mkono.

Kupitia app hii unaweza kuweka maandishi kwenye PDF ambapo utaweza kuprint maandishi hayo kwa urahisi kupitia app hii au kwa kutuma file hilo la PDF.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use