Ukweli ni kwamba muziki mzuri unapendwa na kila mtu, uwe ni kijana ua hata mzee lazima kwa namna moja ama nyingine unapenda kusikiliza muziki.
Kuliona hili leo nimekuletea makala fupi sana ambayo itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa wewe mpenzi wa muziki au hata msanii, au mtengenezaji wa muziki ambaye unasambaza nyimbo zako kwa njia ya mtandao.
Kupitia makala hii nitakuonyesha hatua kwa hatua jinsi ya kuweza kubadilisha link ya muziki kutoka kwenye mtandao mmoja kwenda kwenye mtandao mwingine kwa urahisi ndani ya sekunde mbili.. Kitu cha muhimu hakikisha unayo Internet kwenye simu au kompyuta yako na moja kwa moja utakuwa upo tayari kusikiliza nyimbo yoyote kupitia mtandao wowote unaopendelea.
Hatua za Kufuata
Kwa kuanza unatakiwa kutembelea tovuti ya odesli, baada ya hapo utaweza kuona sehemu ya kuweka link kwa juu kabisa ya tovuti hiyo.
Baada ya hapo sasa chukua link kutoka mtandao wowote unao sambaza muziki, kwa mfano YouTube, Spotify, Apple Music au mtandao wowote. kisha moja kwa moja paste kwenye sehemu ya kuweka link kwenye tovuti ya odesli.
Baada tu ya kuweka link moja kwa moja utaweza kuona list ya mitandao mingine ambao inayo nyimbo hiyo, unaweza kusikiliza nyimbo au download nyimbo kutoka kwenye mtandao wowote kati ya iliyo ainishwa kwa kubofya link husika.
Njia hii inaweza kumsaidia sana msanii kushare nyimbo yake kupitia mitandao ya kijamii, huku akitoa ruhusa kwa nyimbo hiyo kusikilizwa kwenye mtandao wowote unao sambaza muziki.
Na hiyo ndio njia rahisi ya kuweza kusambaza au kubadilisha link ya muziki kutoka mtandao mmoja kwenda mtandao mwingine. Natumaini njia hii inaweza kusaidia sana kwa wale wenye uhitaji. Mpaka siku nyingine endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.