Kampuni moja ya teknolojia ya Touchjet imetengeneza kifaa kipya chenye uwezo wa kubadilisha TV yako na kuwa Touchscreen yenye kutumia Android. Kifaa hicho ambacho kinafanya kazi kama projector kwa sasa tayari kipo sokoni kikiwa kinauzwa kwa dola za marekani $299.99.
Akieleza jinsi kifaa hicho kinavyotumiaka mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo alisema, kifaa hichi hutumika kama projector ndogo ambayo hutumia TV yako ili kuweza kuonyesha picha ambazo mtumiaji ataweza kutumia picha hizo kwa kugusa au kwa kutumia programu maalum ya smartphone kama remote ya TV yenye kifaa hicho.
Kifaa hichi cha Touchjet Wave kina sifa za RAM ya GB2 na kinauwezo na ukubwa wa GB16 kikiwa kinatumia Android 4.4 KitKat, hii ikiwa inakupa uwezo wa kuhifadhi programu mbalimbali za Android tayari kwa kutumia kwenye TV yako.
Kwa sasa kifaa hicho kinapatikana kupitia kwenye maduka ya marekani ya Best Buy kwa tanzania kama unahitaji kifaa hichi unaweza kununua kupitia mtandao wa Best Buy, lakini itakubidi kusubiri mpaka wiki ijayo ambapo ndio kampuni hiyo itaanza kusafirisha kifaa hicho.