Sehemu maarufu ya Facebook Stories ambayo iliyotoka kwa mara ya kwanza kwenye programu za facebook za Android na iOS sasa inakuja kwenye facebook ya kompyuta.
Kama tunavyojua sehemu ya stories hua pekee kwenye programu za simu za facebook, lakini hivi karibuni kampuni hiyo imethibitisha kwamba sasa iko kwenye hatua za mwisho za majaribio ili kuileta sehemu hiyo kwenye tovuti yao.
Akiongea na wataalamu kutoka Facebook mwandishi wa gazeti la mtandaoni la Techcrunch amesema kuwa facebook imekubali na kusema sehemu hiyo ina tarajiwa kutoka hivi karibuni na alisema kuwa wamepanga kuweka sehemu hiyo upande wa kulia juu kabisa pale ambapo panatokea siku za kuzailiwa za marafiki kwenye mtandao huo wa kijamii.
Sehemu ya Facebook Stories Sasa Kuja kwenye Tovuti ya Facebook pic.twitter.com/slmdvNkblM
— Tanzania Tech (@tanzaniatech) August 4, 2017
Kwa sasa usishangae kuona sehemu hii kwa baadhi ya watumiaji ikiwa kama sehemu ya majaribio ya facebook ili kuweza kuleta sehemu hiyo kwenye tovuti yake.
Sehemu ya stories ilianza kuwa maarufu kwenye programu ya Snapchat na baadae kuigwa na mitandao kama Instagram, Facebook na baadae kuja kwenye programu ya WhatsApp. Aidha sehemu hiyo inaonekana kufanya vizuri kwenye programu za Instagram pamoja na WhatsApp huku ikiwa ina suasua kwenye programu za Facebook, labda mabadiliko haya yanaweza kufanya sehemu hiyo kuanza kutumiwa zaidi kwenye mtandao wa Facebook.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.
Chanzo : The Verge