Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya AT&T Kununua Time Warner Kwa Dollar Billion $85.5

Kampuni ya AT&T ya marekani imetangaza kununua kampuni ya Time Warner yenye channel za HBO, Warner Bros, CNN, DC Comics na TNT
AT&T AT&T

Kampuni yenye makao yake makuu nchini marekani ya AT&T Jumamosi iltangaza rasmi kununua kampuni ya Time Warner, Time Warner ndio kampuni mama yenye channel (cable channel) za CNN, TNT, na HBO pia vilevile kampuni hiyo inamiliki studio za filamu za Warner Bros, TV studio pamoja na Castle Rock Entertainment.

Kampuni hiyo ya simu pamoja na usambazaji wa internet ya AT&T imekubali kulipa asilimia 50 ya pesa cash na asilimia 50 ya hisa za kampuni yake, hivyo pale makubaliano yatakapo kamilika wamiliki wa hisa za kampuni ya Time Warner watabakiwa na hisa za kampuni yao kwa asilimia 14.4 na watakuwa na hisa kwenye kampuni ya AT&T kwa asilimia 15.7.

Advertisement

Makubaliano hayo kwa sasa yametumwa kwa wamiliki wa hisa za kampuni hizo pamoja na ukaguzi wa serikali ya marekani (government regulatory) ili kufanyiwa uchunguzi na kupitishwa hapo baadae, Hata hivyo kampuni ya AT&T imetangaza kuwa inategemea makubaliano hayo kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka 2017.

Kama unataka kupata habari zaidi za teknolojia unaweza kujiunga na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use