Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Zifahamu Hizi Hapa Apps Zote Nzuri Kutoka Tanzania Tech

Hizi hapa ndio baadhi ya apps zilizo tengenezwa na Tanzania Tech
Zifahamu Hizi Hapa Apps Zote Nzuri Kutoka Tanzania Tech Zifahamu Hizi Hapa Apps Zote Nzuri Kutoka Tanzania Tech

Kwa muda sasa Tanzania Tech tumekuwa tukijikita kwenye ulimwengu wa teknolojia kwa namna mbalimbali ikiwa pamoja na kutengeneza programu mbalimbali kwaajili ya kompyuta pamoja na tovuti mbalimbali.

Kupitia hapa leo tumeona ni bora tufahamishane wote kwa ujumla kuhusu programu hizi ambazo wengi wenu najua mtakuwa hamzijui, najua leo ni siku ya mapumziko na bila kukupoteza muda mwingi basi twende moja kwa moja tukafahamu apps hizi.

Advertisement

Gazeti App

Kupata habari imekuwa ni rahisi sana siku hizi, hii inatokana na kuwepo kwa vyanzo vingi vya habari kiasi kwamba ni lazima utaweza kupata habari kupitia vyanzo hivyo. Lakini wote tunajua ni ngumu sana kupata habari kwa ukamilifu kwa kuwa haiwezekani kutembelea tovuti zote hizo kwa pamoja ndio maana tunakuletea App ya Gazeti.

Gazeti ni App itakayokupa uwezo wa kusoma Magazeti ya leo pamoja na habari mbalimbali kwa urahisi kutoka tovuti mbalimbali, Mbali na tovuti app ya Gazeti inakupa uwezo wa kusikiliza radio pamoja na idhaa za kiswahili kutoka nchi mbalimbali.

Gazeti App pia inakupa urahisi wa kuangalia TV mbalimbali za hapa nchini Tanzania na nje ya nchi, kifupi ni kwamba Gazeti App inakupa habari zote za Ndani ya Tanzania kwa haraka na kwa urahisi.

Nyubeat

Nyubeat ni app nzuri inayokupa uwezo wa kudownload pamoja na kusikiliza nyimbo mpya za Tanzania audio na video. App hii ni rahisi kutumia na utaweza kudownload nyimbo mpya kutoka kwa wasanii wote wa Tanzania, pia utapata taarifa pale nyimbo mpya itakapo toka.

Pakua app ya Nyubeat kwani itaendelea kuboreshwa kila siku huhakikisha hupitwi na nyimbo yoyote mpya.

Cheka Point

Kama wewe ni mpenzi wa video fupi na picha basi app ya Cheka Point ni app nzuri sana kwako, app hii ni nzuri kwa sababu inakupa uwezo wa kupakua video na picha moja kwa moja na pia vilevile unaweza ku-upload picha na video moja kwa moja kupitia kwenye app hii. Unaweza kujaribu app hii kwa sasa inayo vichekesho zaidi ya 500.

Klik Loko

KLIK LOKO ni Soko namba moja Tanzania ambalo limejikita katika kuuza na kununua vifaa vya kielectroniki Tanzania. Kama unataka kununua Simu, TV, Kompyuta au kifaa chochote cha kielectroniki basi hapa ndio sehemu sahihi.

Kupitia KLIK LOKO utaweza kununua au kuuza kifaa chako kwa haraka na kwa urahisi bila kupoteza muda, tofauti na masoko mengine ya kuuza na kununua mtandaoni wa KLIK LOKO unakupa uwezo wa kupata wateja kwa urahisi na haraka bila kupoteza pesa nyingi mtandaoni.

Simu QR

Simu QR itakusaidia kutengeneza QR Codes pamoja na Barcodes kwa Urahisi kupitia simu yako ya mkononi. Mbali na kutengeneza QR Codes na Barcodes App hii pia itakusaidia kusoma Codes hizo kwa kutumia kamera ya simu yako ya mkononi. Simu QR ni rahisi kutumia na inahifadhi kumbukumbu za codes zako moja kwa moja kuptia simu yako ya mkononi.

Tanzania Tech

Tanzania Tech ni programu ya habari na mafunzo mbalimbali ya Teknolojia, programu hii ina lengo la kufikisha habari na mafunzo mbalimbali ya Teknolojia kwa jamii kwa lugha ya Kiswahili, vile vile Tanzania Tech inasaidia jamii kuelewa kwa undani kuhusu Teknolojia mpya kutoka ndani na nje ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Na hizo ndio App ambazo zimetengenezwa na Tanzania Tech, kwa sasa bado tuko kwenye jitihada za kuwaletea apps nyingine nzuri. Kama unataka kujua apps nyingine nzuri kwa simu zilizopo rooted unaweza kusoma hapa. Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use