Simu kutokudumu na Chaji ni tatizo la simu nyingi sana za Android siku hizi, lakini pamoja na tatizo hili kuongezeka kila siku ni kweli kuwa matumizi ya simu nayo pia yamekuwa makubwa sana na pengine hii ndio sababu ya simu nyingi kutokuwa na uwezo wa kudumu na chaji kwa muda mrefu.
Lakini kama kwa namna yoyote umekuwa ukiona matumizi yako ni ya kawaida na bado simu yako ya Android inaisha chaji kwa haraka sana basi ni wakati wa kujaribu njia nyingine kama hizi za Apps nzuri za kukusaidia kufanya simu yako idumu na chaji kwa muda mrefu.
Njia ya kutumia apps hizi ni nzuri kwani inakusaidia kuweza kusitisha baadhi ya kazi ambazo zinafanywa na simu yako ambazo zinakuwa hazina ulazima kwa namna moja ama nyingine. Basi bila kupoteza muda let’s get to it.
AccuBattery
AccuBattery ni moja kati ya App nzuri sana, App hii inauwezo wa kukusaidia kufanya simu yako idumu na chaji kwa muda mrefu, app hii pia inauwezo wa kukuonyesha mambo mbalimbali kama vile muda gani battery yako inatumia kujaa au kuisha pale unapoichaji, pia ina kuonyesha kiasi cha chaji kinacho tumiwa na kila app kwenye simu yako.
Amplify
Kama wewe ni mmoja wa watu wenye simu ambazo ziko rooted basi na hakika utapenda app hii ya Amplify. App hii inauwezo wa kuangalia mfumo mzima wa android na kuonyesha app zinazotumia chaji sana na ikiwa pamoja na njia za kuweza kuzima apps hizo. Kama unasimu ambayo iko rooted basi jaribu app.
Greenify
Kama wewe ni mfuatiliaji wa tovuti ya tanzania tech nadhani utakuwa umesha sikia tukitaja app hii mara nyingi sana. App hii ni nzuri sana ya kuweza kufanya simu yako idumu na chaji. App hii inauwezo mzuri wa kuzima apps ambazo zinatumia chaji nyingi na kufanya simu yako kudumu na chaji zaidi.
Avast Battery Saver
Avast battery saver ni app nyingine nzuri sana ya kufanya simu yako kudumu na chaji, App hii inauwezo wa kuonyesha kiasi cha chaji kinacho tumiwa na apps mbalimbali kwenye simu yako, vilevile app hii inakupa uwezo wa kuzima apps hizo kwa kubofya kitufe kimoja tu.. Kama unatafuta app nzuri na rahisi kutumia basi unaweza kutumia app hii.
Gsam
Gsam ni app nzuri kwa wale wanapenda kujua zaidi kuhusu tabia za apps mbalimbali kwenye simu zao. App hii inakupa uwezo wa kujua kuhusu app zinazo tumia chaji kwa wingi ikiwa pamoja na settings mbalimbali ambazo labda umeseti kwenye simu yako ambazo zinatumia chaji kwa wingi.
Kaspersky Battery Saver
App nyingine nzuri ambayo itakusaidia kufanya simu yako idumu na chaji ni app ya kaspersky battery saver. App hii ni nzuri na kweli inauwezo mkubwa wa kufanya simu yako iweze kudumu na chaji kwa muda mrefu.
Na hizo ndio apps nilizo kuandalia kwa siku ya leo, kama unataka kujua apps nyingine nzuri za kuongeza ulinzi kwenye simu yako ya Android basi soma makala hii hapa. Kwa habari zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.
Iko poa sana aisee nimeipenda
Karibu