Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Apps (5) za Muhimu Kuwa Nazo Kwenye Android TV (2024)

Apps hizi ni muhimu sana kama unamiliki TV yoyote yenye mfumo wa Android
Apps (5) za Muhimu Kuwa Nazo Kwenye Android TV (2024) Apps (5) za Muhimu Kuwa Nazo Kwenye Android TV (2024)

Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa Android TV basi makala hii ni maalum kwa ajili yako, kupitia makala hii nitaenda kuonyesha apps muhimu kuwa nazo kwenye TV yako yenye mfumo wa Android.

Apps tutakazo onyesha hapa ni tofauti kabisa na zile ambazo tulizionyesha mwaka 2022, hivyo hakikisha unasoma makala hii hadi mwisho ili kujua apps zote. Pia bado apps ambazo tulizitaja kwenye makala iliyopita ni bora hivyo unaweza pia kutumia apps hizo kwenye TV yako.

Advertisement

atvTools

Apps (5) za Muhimu Kuwa Nazo Kwenye Android TV (2024)
App ya atvTools

atvTools ni app muhimu sana kwani itakusaidia kufanya mambo mbalimbali kwenye TV yako kwa kutumia simu yako ya mkononi ya Android. Kupitia app hii unaweza kudownload apps kupitia simu yako na zitaonekana moja kwa moja kwenye TV yako, utaweza kutumia simu yako kama Remote, utaweza kutuma mafile yaliyo kwenye simu yako kwenda kwenye TV yako, utaweza kuinstall apk kutoka kwenye simu yako na apps ita onekana kwenye TV na mambo mengine mengi.

atvTools
Price: Free

Local Send

Apps (5) za Muhimu Kuwa Nazo Kwenye Android TV (2024)
App ya Local Send

Kama kwa namna yoyote unahitaji kutuma mafile makubwa kutoka kwenye simu yako kwenda kwenye TV basi app hii ni muhimu sana kuwa nayo kwenye TV yako. Kupitia app hii unaweza kutuma files kwa haraka kutoka kwenye simu (Android na iOS), kompyuta (za aina zote) kwenda kwenye TV yako.

Browser

Apps (5) za Muhimu Kuwa Nazo Kwenye Android TV (2024)
App ya Browser

Kama unataka kivinjari browser nzuri na bora kwenye TV yako basi app hii ni muhimu sana kuwa nayo kwenye TV yako. Mbali ya kuwa zipo browser nyingi sana ikiwa pamoja na zile zinazokuja na TV moja kwa moja, lakini zote hazifanani na browser hii kwani ni browser bora sana. Mbali na hayo pia unaweza kuendesha browser hii kupitia simu yako, yaani kila unacho kifanya kitakuwa kinaonekana kwenye TV moja kwa moja.

Browser
Price: Free

Aerial Views screensaver

Apps (5) za Muhimu Kuwa Nazo Kwenye Android TV (2024)
App ya Aerial Views screensaver

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanatumia TV yako kama pambo sebuleni kwako au hata ndani ya studio yako basi app hii ni bora sana kwako. App hii ina kusaidia kuweka Video za 4K au video zozote kama screensaver. App hii ni nzuri sana kuwa nayo.

Just (Video) Player

Apps (5) za Muhimu Kuwa Nazo Kwenye Android TV (2024)
App ya Just (Video) Player

Wote tunajua kuwa VLC ni moja ya player bora sana, lakini kwa bahati mbaya haifanyi kazi kwenye baadhi ya Android TV. Kuliona hili nimekuletea app bora ambayo ni Video Player kwa ajili ya TV yako app hii ina karibia sifa zote za VLC ikiwa moja na uweza wa kuplay format zote kama MP4, MKV, VOD na format nyingine nyingi.

Just (Video) Player
Price: Free

Na hizo ndio apps 5 muhimu ambazo unaweza kutumia kwenye TV yako yenye mfumo wa Android, Kama unataka kujifunza zaidi hakikisha unasoma hapa jinsi ya kuangalia channel zaidi ya 5000+ kupitia Android TV. Kukaa karibu na sisi unaweza kupakua app ya Tanzania Tech kupitia Play Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use