Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Programu za Kusaidia Kurudisha Picha na Video Zilizofutika

Zifahamu hizi hapa programu zinazoweza kurudisha picha na video zilizofutika
Programu za kusaidia kurudisha picha na video zilizo futika Programu za kusaidia kurudisha picha na video zilizo futika

Kama wewe ni mmoja wa watu wanaotumia smartphone basi ni wazi kwa namna moja ama nyingine umewahi kukutana na kadhia ya kupoteza data zako kwenye simu yako kwa bahati mbaya, iwe ni mtu amefuta vitu vyako kwa bahati mbaya au umefuta wewe mwenyewe, ukweli ni kwamba hali hii inaudhi sana hasa pale unapokosa msaada wa jinsi ya kupata picha au video zako.

Kwa sababu unafahamu tovuti ya Tanzania Tech basi usishindwe tena kupata data zako kwani leo tunaenda kukujuza programu mbalimbali ambazo zinaweza kukusaidia kurudisha picha au video zako moja kwa moja. Programu hizi zipo zile ambazo ni kwa ajili ya kompyuta na zipo zile ambazo ni kwa ajili ya simu za Android kwa ujumla zote zina uwezo wa kufanya kazi vizuri kwa asilimia 100. Basi bila kukuchosha twende tukangalie programu hizi.

Advertisement

1. DiskDigger

App ya DiskDigger kurudisha picha na video zilizo futika

DiskDigger ni moja kati ya app nzuri sana ya Android ambayo itakusaidia kurudisha picha na video zako kwa urahisi sana. App hii inakuja na matoleo mawili, toleo la bure na toleo la kulipia huku toleo la bure likiwa na uwezo wa kurudisha picha na video pekee zilizo futika, wakati toleo la kulipia lina uwezo wa kurudisha hadi meseji pamoja na file mbalimbali. App hii ni nzuri sana ya kurudisha vitu vilivyo futika kwenye Android, kujua jinsi ya kutumia unaweza kusoma zaidi hapa.

2. Dr Phone

Dr Phone kurudisha picha na video zilizo futika

Kama wewe ni mmoja ya watu wenye kompyuta (Windows au Mac), basi una bahati sana kwani programu hii inauwezo mkubwa sana wa kurudisha vitu vyote vilivyo futika kwenye simu yako kwa bahati mbaya. Mbali ya kurudisha vitu vyote programu hii inauwezo wa kufanya mambo mengine mbalimbali ambayo najua lazima utapenda. Unaweza kujua zaidi kwa kusoma hapa.

3. Gihosoft

Gihosoft kurudisha picha na video zilizo futika

Gihosoft ni aina nyingine ya programu ambayo unaweza kutumia kurudisha picha au video zilizopotea, uzuri wa programu hii ni kuwa unaweza kurudisha video na picha mbalimbali kama vile picha zilizopotea kwenye WhatsApp, Viber na programu nyingine kwenye simu yako. Programu hii ni ya kompyuta hivyo unahitajika kuwa na kompyuta (Windows au Mac) pamoja na waya wa USB wa simu yako ndipo uweze kutumia.

4. MiniTool Android Recover

MiniTool kurudisha picha na video zilizo futika

MiniTool Android Recovery ni programu nyingine nzuri sana kwa kurudisha picha na video zilizo futika, uzuri wa programu hii ni kuwa unaweza kuitumia bure kabisa bila kulipa na unaweza kurudisha vitu mbalimbali kwenye simu yako kama vile, Picha na video za WhatsApp, picha na video za Viber, Meseji (SMS), Coll Logs, Doc pamoja na mafile mbalimbali. Programu hii ni bure kabisa na kama unayo kompyuta basi unaweza kuijaribu sasa, unahitaji tu waya wa USB pamoja na simu yako ya Android.

5. Recuva File Recovery

Recuva File Recovery kurudisha picha na video zilizo futika

Recuva File Recovery ni moja kati ya programu zenye uwezo mkubwa sana wa kurudisha vitu vilivyo futika. Programu hii inauwezo wa kurudisha file mbalimbali kwenye simu za Android na iOS na pia inauwezo wa kurudisha data zilizo futika hata kwenye memory card. Ili kutumia Recuva File Recovery unahitaji kuwa na waya wa USB pamoja na simu yako ya Android au iOS.

6. EaseUS MobiSaver

EaseUS MobiSaver kurudisha picha na video zilizo futika

EaseUS MobiSaver ni app nyingine ya Android yenye uwezo wa kurudisha picha na video zilizo futika. Uzuri wa app hii ni kuwa haitaji kompyuta hivyo unaweza kutumia kwenye simu yako ya Android hivi sasa, kitu cha tofauti kuhusu app hii ni kuwa inahitaji simu yako iwe iko rooted ndipo uwezo kupata vitu mbalimbali ambavyo vimefutika kwenye simu yako.

7. FonePaw Android Data Recovery

FonePaw Android Data Recovery kurudisha picha na video zilizo futika

Kama hadi sasa bado ujafanikiwa njia moja ya kurudisha picha na video zako zilizo futika kwa bahati mbaya basi unaweza kujaribu programu hii ya FonePaw Android Data Recovery. Programu hii inauwezo wa kurudisha vitu mbalimbali ikiwa pamoja na SMS, Call Logs, picha za WhatsApp na file zingine mbalimbali. Programu hii ni rahisi sana kutumia na unaweza kuitumia kama unayo kompyuta pamoja na waya wa USB wa simu yako.

Na hizo ndio programu ambazo unaweza kutumia kwa namna moja ama nyingine kurudisha data zako kwenye simu yako, Kama ulikuwa unashindwa kurudisha vitu vyako vilivyofutika kwenye simu yako na uhakika moja ya programu hizi zinaweza kusaidia kwa namna yoyote. Kama unataka kujua programu zaidi ambazo zinaweza kukusaidia kwenye maisha yako ya kila siku unaweza kusoma hapa.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use