Zipo faida nyingi sana za kuroot simu yako, lakini vilevile hakuna kizuri kisichokuwa na kasoro na kwa sababu unapo root simu yako unapoteza warrant inayokuja na simu yako ni vyema kuwa makini sana pale unapo amua kuroot simu yako.
Tukiachana na hayo, kupitia makala hii leo nimekuandalia apps mbalimbali za Android ambazo unaweza kutumia ili kuroot simu yako kwa urahisi na haraka. Apps hizi ni app za android na huna haja ya kutumia kompyuta zaidi ya kufuata maelekezo ndani ya app hizo.
Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye apps hizi, kumbuka ni muhimu kuwa makini usije kuharibu simu yako.
TABLE OF CONTENTS
CF-Auto-Root
CF-Auto-Root inaelezewa kama njia ya kuroot simu kwa watu ambao hawajui kuroot simu. Kupitia app hii Inachofanya ni kuwezesha SuperSU ili uweze kutumia root kwenye simu yako. App hii inaroot kwa urahisi simu za Samsung. Unaweza kusoma kuhusu app hii hapa, pia unaweza kudownload kupitia link hapo chini.
Framaroot
Framaroot ni app nyingine ya kuroot simu, app hii inaweza kuroot simu zenye mfumo wa Android kuanzia Android 4.0+ na kuendelea. App hii haiwezi kuroot simu nyingi sana za hivi sasa lakini unaweza kujaribu app hiyo. Unaweza kusoma hapa kujua zaidi kuhusu jinsi ya kutumia Framaroot. Unaweza kudownload app hii kupitia link hapo chini.
KingoRoot
KingoRoot ni app nyingine inayoweza kusaidia kuroot simu yako kwa urahisi, app hii inaweza kuroot simu nyingine zenye mfumo wa Android Nougat na kama unatumia simu yenye mfumo huo basi unaweza kujaribu mfumo huu. Unaweza kusoma zaidi kuhusu app hii hapa au download kupitia link hapo chini.
Root Master
Root Master ni app nyingine nzuri ya kuroot simu, app hii ni rahisi kutumia na ni moja kati ya app ambayo pengine ni bora kwenye list hii. Tatizo la app hii haijawa updated kwa muda sasa toka mwaka 2017 hivyo inawezekana kuwa simu nyingi za sasa ziweze kuroot kwa kutumia njia hii. Unaweza kujaribu app hii kupitia link hapo chini.
Na hizo ndio app za kuroot simu yako ya Android, kumbuka app hizi zinaweza kuroot simu yako au zinaweza kushindwa, kutu cha muhimu hakikisha unajaribu app hizi au unasoma maelezo kabla ya kuamua kutuimia programu yoyote ya Android kati ya hizi.
Kama unataka kujua zaidi kuhusu kuroot simu unaweza kusoma hapa kujua hatua za kuroot simu ikiwa pamoja na faida na hasara za kuroot simu.
mimi nina cm ya tecno pop2 pawa lakini kila app imegoma kroot zinafel t nifanyej
Simu Ana ya VIWA Nima sau pin patine