Hizi Hapa Apps Nzuri Kwaajili ya Watafutaji wa Ajira Rasmi

Apps hizi zitakusaidia kupata ajira kwa kufanya mambo ya msingi
Hizi Hapa Apps Nzuri Kwaajili ya Watafutaji wa Ajira Rasmi Hizi Hapa Apps Nzuri Kwaajili ya Watafutaji wa Ajira Rasmi

Najua kwa sasa ni kipindi cha mwaka wa ambapo wahitimu wanamaliza, hivyo watu wengi sana hasa walio maliza elimu ya juu wako kwenye hatua za awali za kutafuta ajira. Kuliona hili leo nimekuletea list ya apps ambazo zinaweza kurahisisha utafutaji wako wa ajira hasa kama unatafuta ajira rasmi.

Kitu cha muhimu cha kuzingatia ni kuwa, naposema “ajira rasmi” hapa nina maanisha ajira za ma-ofisini au ajira zote zile ambazo zinahitaji ujuzi wa kusomea ajira hizi nyingi huwa unahitaji kufuata hatua fulani za maombi ili kuweza kupata ajira husika. Lakini pia hata kama wewe sio mtafutaji wa ajira rasmi makala hii pia inaweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie apps hizi.

Advertisement

Kama unatafuta ajira hatua ya kwanza ni kutafuta ajira yenyewe, kupitia app ya Zoom Tanzania utaweza kupata uwezo wa kupata ajira mbalimbali moja kwa moja kupitia app hii. Moja ya sehemu muhimu kwenye app hii ni pamoja na sehemu ya kusave kazi kwa ajili ya ku-appy baadae pamoja na uweza wa kupata ujumbe pale kazi mpya itakapo wekwa kwenye tovuti hiyo.

Ukweli ni kwamba hakuna ambaye anatafuta ajira alafu hapitii hatua ya kuandika CV, app hii ya Resume Builder itakusaidia kutengeneza CV kwa haraka na kwa urahisi. Uzuri wa app hii ni kuwa inauwezo wa kutengeneza CV za kisasa huku ukiwa na uwezo wa kutoa CV uliyo tengeneza kuwa kwenye mfumo wa PDF. Hivyo kama unahitaji CV nzuri ya haraka itakayo kusaidia kupata ajira basi app hii ni nzuri sana kwako.

Baada ya kuandika CV nzuri na kupata ajira hatua inayofuata ni kuitwa kwenye Interview, hapa ndio app hii ya Interview Question and Answers inakuwa ya muhimu kwako. App hii inakuja na maswali yote ya muhimu ambayo yanayoulizwa kwenye interview nyingi za ajira rasmi. Kama unategemea kuingia kwenye ajira rasmi siku za karibuni basi app hii ni nzuri sana kwako.

TZ Salary Calculator

Mara baada ya kupata kazi hatua inayofuata ni mshahara na hapa ndipo app hii ya TZ Salary Calculator inapokuwa na umuhimu. App hii inakusaidia kukokotoa kiasi cha makato ambayo unakatwa kwenye mshahara wako ili kufahamu mshahara kamili. Kupitia app hii unaweza kukokotoa Gross Salary, P.A.Y.E, Pension pamoja na Net Salary.

Kama app hiyo hapo juu haitoshi basi unaweza kujaribu app hii ambayo yenyewe inakupa nafasi ya kukokotoa mpaka mkopo wa elimu ya juu kama unao ikiwa pamoja na makato mengine kama pension na makato mengine ya muhimu.

The 48 Laws of Power

Baada ya kufanikiwa kupata mshahara vizuri na kujua makato yako ni wazi sasa unataka nyongeza ya mshahara, sasa hapa ndipo app hii inapokuwa ya muhimu. App hii ya 48 Laws of Power itakusaidia sana kuishi na wafanyakazi wenzako vizuri sana na itakusaidia kufika kileleni kwa haraka sana, app hii inakuja na sheria 48 ambazo hizo zitakusaidia sana kwenye maisha yako kwa ujumla na utajikuta kila mtu anakupenda na kukuheshimu na wewe uliopo kazini app hii itakusaidia sana mimi imenisaidia na inaendelea kunisaidia hadi sasa.

How To Write A Report

Sasa najua kuwa ili kutimiza majukumu yako ya kazi ni lazima kuandika ripoti, iwe ni kila siku, kila wiki, kila mwezi au kila mwaka app hii ni muhimu sana kwako. App hii itakufundisha jinsi ya kuandika ripoti mbalimbali hatua kwa hatua, mbali ya yote ni kuwa utaweza kujifunza kuandika ripoti za karibia kila kitu. Kama wewe ni mwajiriwa mpya basi app hii ni nzuri sana kwako.

Na hizo ndio apps nzuri ambazo zinaweza kukusaidia sana kwako wewe mtafutaji wa ajira rasmi, kama unataka kutafuta ajira basi unaweza kusoma hapa kujua tovuti bora ambazo zinaweza kukusaidia kuweza kupata ajira kwa haraka.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use