Ni kweli kwamba hizi Android TV zimekuwa zinapatikana kwa bei rahisi sana kiasi kwamba unaweza kupata Android TV kuanzia TZS 300,000 na kuendelea. Anyway, kuhusu bei tufanye hii ni mada ya siku nyingine.
Kwa siku ya leo ningependa ufahamu apps za muhimu kuwa nazo kwenye Android TV yoyote, Apps hizi ni muhimu kwa kuwa zitaweza kusaidia sana kufanya mambo kwa urahisi na haraka hivyo kwa maoni yangu naona ni muhimu kwa mtu yoyote mwenye Android TV kuwa nazo kwenye TV yake.
TABLE OF CONTENTS
App Muhimu Kuwepo Kwenye Android TV Yoyote
Kwa kuanza ni vizuri kujua kuwa unaweza kudownload apps hizi kupitia link chini ya maelezo ya kila app, pia baadhi ya apps hizi zinapatikana kwenye soko la Play Store ndani ya TV yako, lakini pia baadhi ya apps ni lazima kutumia apk. Basi kwa kusema hayo twende tuka angalie app ya kwanza.
Bluetooth Settings
Moja kati ya sehemu ambayo usumbua sana kwenye TV za Android ni pamoja na sehemu ya Bluetooth. Ni vizuri ufahamu kuwa TV nyingi zinakuja zikiwa hazina sehemu ya kuzima Bluetooth hii ni kwa sababu uhitaji wa Bluetooth ni mkubwa sana kwenye TV hizi.
Kupitia App ya Bluetooth Settings unaweza kuongeza kipengele ambacho kitakusaidia kuzima bluetooth ikiwa pamoja na kufanya settings mbalimbali kwenye sehemu ya Bluetooth ili kuongeza usalama zaidi na usumbufu wa mtu kuunganisha Bluetooth kwenye TV yako bila ruhusa.
Nova Video Player
Ni wazi kuwa Android TV zote zinakuja na Video Player lakini ukweli nakwambia hakuna Video Player ambayo itazidi hii Nova Video Player. App hii inakuja na muonekano mzuri sana na uwezo wa kupanga movie yenyewe bila kutumia Internet.
Mbali na hayo utaweza kutafuta subtitle ya movie yoyote online kwa urahisi bila kutumia app nyingine yoyote, pia app hii itaweza kuchagua ni movie gani uangalie bila kutumia Internet. Ukweli ni kwamba hii ni app muhimu sana kwenye TV yako yenye kutumia mfumo wa Android.
Send files to TV
Kama umekuwa ukitaka kutuma kitu chochote kutoka kwenye simu yako kwenda kwenye TV yako basi Send files to TV ni app muhimu kuwepo kwenye TV yako. Najua kuna wakati unataka kutumia APK kutoka kwenye simu yako kwenda kwenye TV yako ya Android hivyo hapa ni muhimu kutumia app hii. App hii ni muhimu sana, niamini utahitaji kuwepo nayo hapo baadae.
Unaweza kuangalia Video hapa kujua jinsi ya kutumia app hii kupitia simu yako pamoja na kwenye TV yako ya Android.
Puffin For Android TV
TV zote za Android zinakuja na browser lakini ni wazi kuwa browser hizo zinakuja na uwezo mdogo wa kufungua kurasa mbalimbali, hii ni kwa sababu app nyingi za browser zinazokuja na TV zina muundo mbaya na hivyo kufanya kazi ya kufungua kurasa mbalimbali mtandaoni kuwa ngumu sana. Mbali na hayo pia zingine huja na lugha ambazo sio kingereza.
Kupitia Puffin Browser for TV utaweza kufungua kurasa mbalimbali kwa urahisi na haraka na pia utaweza kutumia apps mbalimbali kwa urahisi moja kwa moja kwenye browser hii.
Uzuri ni kuwa app hii inapatikana kwenye soko la Play Store la Android TV hivyo utaweza kupata kwa app hii kwa kutafuta jina la app hii kwa urahisi kwenye TV yako kupitia Play Store.
FX File Explorer
Ni wazi kuwa unapokuwa unatumia TV ya Android ni lazima kuwa na file manager, moja kati ya app ambayo naweza kushauri utumie kwenye TV yako ni FX File Explorer. App hii ni bora kwa kuwa haina matangazo na itakusaidia sana hasa pale unapo hitaji kutafuta aina fulani ya mafaili ya muhimu uliyotuma au kudownload kwenye TV yako.
Kizuri zaidi kuhusu app hii ni kuwa app hii haina matangazo kabisa hivyo unaweza kutumia bila kuwa na wasiwasi wa kupata matangazo mengi hasa pale unapo unganisha TV yako na Internet.
Aptoide TV
Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya apps ambazo nimezitaja hapo juu hazipo kwenye soko la Play Store la Android TV, lakini asante kwa Aptoide TV sasa unaweza kupata apps nyingi zaidi kwenye TV yako. Aptoide TV ni soko la Apps kama ilivyo Play Store, lakini soko la Aptoide TV linakuja na apps nyingi zaidi
Utaweza kupata apps nyingi zaidi kwenye soko hilo ikiwa pamoja na urahisi wa kudownload na kuinstall moja kwa moja kwenye TV yako.
TV Usage
App ya mwisho kwenye list hii ni TV usage, app hii ni nzuri sana kama unao watoto nyumbani ambao unataka kuwazuia wasi angalie TV kupitiliza au app fulani. App hii ina uwezo wa kufunga app fulani kwa password, pia unaweza kuzuia muda ambao unataka mtu aweze kutumia TV husika.
Mbali na yote pia unaweza kuona matumizi ya apps mbalimbali kwenye TV yako ikiwa pamoja na ripoti ya siku jinsi TV yako ilivyo tumika ikiwa na apps gani imetumika na kwa muda gani. Kama unao watoto nyumbani basi app hii ni muhimu kuwa nayo kwenye TV yako.
Hitimisho
Kwa leo hizo ndio apps ambazo ni muhimu kuwa nazo kwenye TV yako ya Android. Kumbuka kuwa unaweza kudownload apps hizi moja kwa moja kupitia link kwenye mwisho ya maelezo ya kila app.
Kama unataka kujifunza zaidi kuhusu apps moja kwa moja unaweza kusoma hapa kujua apps ambazo zinaweza kufanya simu yako kuwa janja zaidi. Kwa makala zaidi kama hizi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku, pia subscriber kupitia channel yetu ya YouTube hapa kama unataka kujifunza maujanja mbalimbali kwa vitendo.