Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Application Zitakazo Kusaidia Kutumia Android Kwenye PC

Application Zitakazo Kusaidia Kutumia Android Kwenye PC Application Zitakazo Kusaidia Kutumia Android Kwenye PC

Watu wengi kwa sasa wanatumia application maarufu ya whatsapp lakini inakuaje kama unakuwa hauna smartphone na unaitaji kutumia whatsapp..? swali hili kwa sasa linautatuzi mrahisi sana kwa wale msiojua kwasasa kuna namna nyingi za kukusaidia kutumia application zilizoko kwenye mfumo wa Android, moja kati ya njia hizi ni kwa kutumia software maarufu kama “Android Emulator” application hizi maalumu kwaajili ya PC au Computer zitakusaidia kutumia Android pamoja na application zake zote kama unavyotumia kwenye Simu yako ya mkononi yani Smartphone hii ikiwamo na application ya WhatsApp.

Applicatin hizi zipo za aina nyingi mbalimbali zenye uwezo unaotofautiana na pia zipo zile za bure na pia hata zile za kulipia, application hizi zimeleta urahisi wa kuamishia simu yako ya mkononi ya android katika computer yako hivyo basi leo tutachambua application hizi tano bora zinazo kuwezesha kutumia Whatsapp na application nyingine nyingi kutoka kwenye mfumo wa Android wa simu yako kwenda kwenye PC au Computer yako.

Advertisement

#1. Bluestacks 

Bluestacks

Bluestacks ni moja kati ya application zinazojulikana sana na watu kote duniani application hii itakuwezesha kuinstall whatsapp pamoja na application nyingine nyingi katika computer yako, pia application ni nzuri pia kwa wale wanaotumia Mac PC. Appliaction hii ni rahisi sana kuinstall pamoja na kutumia Bluestack pia imependekezwa na watumiaji wengi sana duniani kuwa ndio application bora kwaajili ya kutumia android kwenye PC yako.

#2. GenyMotion

genymotion

Genymotion ni moja kati ya jina maarufu sana pale unapotaka kutumia android kwenye PC yako application hii pia itakusaidia pale utakaposhindwa kutumia application ya BlueStacks hivyo basi hii ni moja kati ya njia mbadala kama utakua umeshindwa kutumia application ya zingine. Pia application hii ina uwezo mkubwa sana na pia ni ya bure kabisa kuipakua na hautumii mda mrefu kuiweka kwenye PC yako.

# 3. Andy

andyroid

Andy ni application nyingine itakayo kuwezesha kufanya uone kama bado unatumia smartphone yako application hii itakuwezesha kutumia application nyingi mbalimbali za android bure kabisa bila kulipia chochote, watumiaji kote duniani wanasema ni moja kati ya application za bure zenye nguvu zaidi inapokuja katika swala la kutumia android kwenye PC yako.

#4. YouWave

YouWave

Youwave ni application nyingine itakayo kuwezesha kutumia android kwenye PC yako application hii inauzwa kwa kasi kidogo sana cha pesa kitakacho kuwezesha kufaidi application mbalimbali za android moja kwa moja kutoka kwenye pc yako application hii haiitaji kiasi kikubwa cha Ram kwani application hii haina matoleo mapya. Appliaction hii ni nzuri kwa watu wasiojali kulipia kwa wanachokitaka kwani kwa kiasi kidogo cha pesa unaweza kupata raha ya PC yako na kusahau kabisa Smartphone yako.

# 5. VirtualBox

VirtualBox

VirtulaBox sio Android Emulator  bali ni appliaction ya window itakayo kuwezesha kuintall OS ya android kwenye computer yako, kwa kutumia vitual box unaweza kuinstall android kama OS kwenye pc yako na ukaitumia kama unavyotumia window 7, 8 ama window 10 application hii inafaa kama unataka kuweka android kwenye computer yako kama OS ama Operation Systeam.

8 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use