Kama kawaida leo Apple imetangaza mfumo wake mpya wa iOS 11.1 mfumo huu sasa unakuja na maboresho mengi. Maboresho yanayo onekana kwa haraka ni pamoja na ujio wa emoji nyingi mpya pamoja na kurudi kwa App ya 3D Touch app switcher gesture.
Kama unataka ku-update toleo jipya kupitia kifaa chako basi ni vyema kufuata hatua hizi ambazo zitaweza kuelekeza jinsi ya kufanya hivyo. Muhimu kumbuka kuchaji kifaa chako hadi asilimia 50 kabla ya kuanza ku-update, vilevile hakikisha una bando la kutosha angalau GB 1 au zaidi au inaweza kuwa zaidi kutokana na kifaa unachotumia.
- Kwa kuanza ingia kwenye Settings.
- Alafu bofya General > Software Update.
- Subiri kidogo wakati ukurasa huo ukitafuta update kumbuka inaweza kuchukua muda kidogo.
- Baada ya update kuonekana bofya Download and Install.
- Kisha update zitaangaliwa na Apple kisha zitawekwa kwenye kifaa chako.
Lakini kama unataka ku-update kifaa chako kwa toleo hili jipya kwa kutumia programu ya iTunes basi unaweza kupata link za kudownload mafile maalum kulingana na simu yako, kumbuka kuchagua link yenye jina la kifaa chako.
Download iOS 11.1 IPSW Files
- iPhone X
- iPhone 8
- iPhone 8 Plus
- iPhone 7
- iPhone 7 Plus
- iPhone SE, iPhone 5s
- iPhone 6s, iPhone 6
- iPhone 6s Plus, iPhone 6 Plus
- iPad Pro 10.5-inch, iPad Pro 12.9-inch (2nd-Generation)
- iPad 5
- iPad mini 3, iPad mini 4, iPad Air 2
- iPad Pro 9.7-inch
- iPad Pro 12.9-inch
- iPad Air, iPad mini 2
- iPod touch (6th-Generation)
Kama unataka msaada zaidi unaweza kutuandikia kwenye maoni hapo chini. Kwa habari zaidi za teknolojia usisahau kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play Store nasi tutakujuza habari zote za teknolojia kwa haraka zaidi.