Apple Yaongezea Processor, Graphics na Rangi ya Gold Kwenye MacBook

Apple Yaongezea Processor, Graphics na Rangi ya Gold Kwenye MacBook Apple Yaongezea Processor, Graphics na Rangi ya Gold Kwenye MacBook

Siku ya leo Jumanne kampuni maarufu ya Apple ilitangaza kutoa nyongeza ya matoleo mapya la laptop zake za inch 12 za Macbook, kampuni hiyo ilitangaza kwamba imeongeza processor pamoja na graphics kwenye laptop hizo pia vilevile imeongeza rangi ya rose gold kwenye laptop hizo.

Apple iliendelea kutangaza kuwa imeongeza processor aina ya Skylake ambazo zitakua badala ya zile za Intel Core M Broadwell processors ambazo zilikua awali. Pia Model nyingine ya Macbook iliyokuwa inauzwa dollar za kimarekani $1,299 imeongezewa 64-bit 1.1GHz dual-core Intel Core M3 processor pamoja na Turbo Boost mpaka 2.2GHz, 4MB L3 cache, na hard disk ya 256GB na pia Macbook iliyokua inauzwa $1,599 itakua na nyongeza ya 64-bit 1.2GHz dual-core Intel Core M5 processor pamoja na Turbo Boost mpaka 2.7GHz, 4MB L3 cache, na hard disk ya 512GB.

Advertisement

Hata hivyo kampuni hiyo inasema kuwa laptop hizo zimeongezewa uwezo wa kukaa na chaji mpaka masaa 10 kama unatumia wireless internet na masaa 11 kama unaangalia filamu kupitia iTune, amba hiyo ikiwa ni nyongeza ya lisaa limoja kwa kila matumizi ukilinganisha na laptop hizo hapo awali.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use