Apple Yamuajiri Kiongozi wa Zamani wa Kampuni ya Google

Kiongozi huyo alijiuzulu Google hapo jumatatu na leo amehamia Apple
John Giannandrea John Giannandrea

Kampuni ya Google pamoja na kampuni ya Apple zimekua zikijulikana kuwa washindani kwa muda mrefu sana, sasa katika hali ya kushangaza hivi karibuni Google iliamua kufanya mabadiliko ya kiutawala kwenye sekta ya Search and Artificial Intelligence ambapo inasemekana aliyekuwa kiongozi wa sekta hiyo John Giannandrea, alitenguliwa uongozi wake na kupewa kiongozi mwingine ambapo kiongozi huyo alisemekana kupangiwa majukumu mengine.

Katika hali ya kushtusha siku ya Jumatatu kiongozi huyo John Giannandrea, aliyetenguliwa madarakani alitangaza kujiuzulu na kuamua kuondoka kwenye kampuni ya Google. Hata hivyo hivi leo ripoti zinasema John Giannandrea ametangazwa kuajiriwa na kampuni ya Apple huku akiwa kama kiongozi wa sekta ya “Machine Learning and A.I. Strategy“.

Advertisement

Vilevile inaripotiwa kuwa Giannandre atakuwa ni mmoja kati ya viongozi wajuu 16 ambao wanafanya kazi moja kwa moja na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Apple, Tim Cook.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mtandao wa habari wa New York Times ambao unadai kuinyaka barua pepe ya mwenye kiti huyo kwa wafanyakazi wa Apple, inayodai kuwa Tim Cook ameandika kuwa, “uteuzi huo ni wa msingi sana kwani wanategemea kujifunza mambo mengi sana kutoka kwa mfanya kazi huyo wa zamani wa kampuni ya Google”.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use