Kampuni ya Apple imeongeza uwepo wake kwenye mtandao wa Twitter kwa kuongeza account ya twitter kwaajili ya huduma kwa wateja, akaunti hiyo yenye jina @AppleSupport itakua ikitoa info mbalilmbali za kutumia kifaa chako cha Apple pamoja na kuwasaidia watumiaji wa vifaa hivyo.
“Tupo hapa kuwasaidia wateja wetu kwa mambo mbalimbali yahusuyo bidhaa za apple, pia hata kama unaswali linalohusu bidhaa zetu pia tupo hapa kwaajili hiyo pia” Blog ya @Applesupport iliandika hivyo.
Japokua Account hiyo ina masaa machache kutoka kutengenezwa kwake Account hiyo ina Follower zaidi ya 35,000 ikiwa na maswali mbalimbali ya wateja mbalimbali wa vifaa vya Apple.
Hii sio mara ya kwanza kwa kampuni ya Apple kutengeneza account kwa ajili ya kusaidia wateja wake tayari zipo account za Twitter kama @Apple Music Help , @App Store twitter account ambayo ilikwepo kuanzia mwaka 2009.
Hata hivyo kampuni ya apple inaonyesha kuweka miguu yote miwili katika kusaidia wateja wake hasa watumiaji wa mtandao wa Twitter. Hata hivyo habari zinasema kampuni hiyo imepanga kufungua account kama hiyo kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.