Kampuni ya Apple imatangaza hivi leo kusitisha mkusanyiko wa watu kwenye mkutano wake wa WWDC 2020 na badala yake mkutano huo wa utafanyika kupitia mtandaoni.
Kwa mujibu wa tovuti ya Apple, mkutano huo utafanyika mtandaoni kutokana na virusi vya corona ambavyo vina endelea kusambaa nchi mbalimbali. Mkutano wa WWDC ni mkutano muhimu kwa watumiaji na wabunifu wa vifaa vya Apple kwani kupitia mkutano huo Apple huzindua mfumo mpya wa iOS pamoja na kutangaza ujio wa vifaa vipya vya Apple.
“Tuna tegemea mkutano wa WWDC 2020 utafanyika mwezi Juni kwa njia ya ubunifu kwa mamilioni ya watengenezaji na wabunifu ulimwenguni kote, na kuleta jamii nzima ya watengenezaji pamoja na aina mpya ya uzoefu,” SVP Phil Schiller alisema katika taarifa hiyo.
“Hali ya kiafya ya sasa imehitaji tuweze kuunda muundo mpya wa WWDC 2020 ambao hutatoa programu kamili kwa wabunifu na watumiaji wa bidhaa za Apple, hii pia imetupa mwanga mpya kwenye uzoefu wa kujifunza ndani ya jamii yetu yote ya wabunifu. Tutakuwa tukishiriki maelezo zaidi katika wiki zijazo.” ilisema sehemu ya taarifa ya Apple.
Mkutano wa WWDC 2020, unategemewa kufanyika mwezi June na Apple inategemewa kuzindua mfumo mpya wa iOS 14, macOS 10.16, iPadOS, tvOS 14, pamoja na watchOS 7. Pia vilevile Apple inategemea kuzindua bidhaa zake mpya ikiwa pamoja na tetesi kuhudu ujio wa simu mpya ya iPhone ambayo itakuwa inauzwa kwa bei nafuu zaidi.