Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Fahamu Clips Programu Mpya Kutoka Apple Kwaajili ya Video

Hatimaye kampuni ya Apple yazindua programu yake mpya kwaajili ya video
Clips Clips

Leo ilikua ni siku kubwa kidogo kwa wapenzi wa iphone na ipad pamoja na watumiaji wa iOS kwa ujumla kwani kampuni hiyo leo imefanya uzinduzi wa simu zake mpya za rangi nyekundu za iphone pamoja na ipad. Katika muendelezo wa uzinduzi wake kampuni hiyo pia imezindua programu yake mpya inayojulikana kwa jina la Clips.

Clips ni programu ambayo itakupa uwezo wa kutengeneza video fupi ya dakika moja huku ikikupa uwezo wa kuweka vikorobwezo mbalimbali ikiwa pamoja na stiker na mapambo mengine kama hayo. Mpaka sasa watalamu wa mambo wanasema programu hiyo ya clips inafanana na zile za Snapchat, Vine, Instagram na nyingine kama hizo, tofauti iliyopo kwenye programu hiyo ya clips ni kuwa programu hiyo inalazimisha kushare video hizo kupitia iMessage kama ulitengeneza video hiyo na mtu ambaye yupo kwenye phonebook yako.

Advertisement

Vinginevyo programu hiyo itakuruhusu kupost video hizo kwenda kwenye mitandao mengine yoyote unayotaka. Programu hiyo inategemewa kuja hivi karibuni kupitia App Store, kama unataka kujua zaidi kuhusu programu hiyo mpya tembelea tovuti ya apple kujua tarehe ya kuja kwa programu hiyo.

‎Clips
Price: Free

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use