Kampuni ya Apple hivi karibuni imezindua kitabu chake chenye kuonyesha bidhaa zake zaidi ya 450, kitabu hicho ambacho kitakuwa kama zawadi ya christmas kwa watumiaji wa Apple kinategemewa kuanza kuuzwa hivi karibuni.
Kuelewa zaidi kuhusu Kitabu hicho ambacho kimetengenezwa na Apple wenyewe kitakua na picha maridadi za bidhaa mbalimbali za kampuni hiyo zikiwa ziko kwenye hali ya kutengenezwa, hata hivyo kitabu hicho kitakua na picha za bidhaa ambazo zingine na uhakika ulikua ujui kabisa kama kampuni hiyo inatengeneza, picha zilizoko kwenye kitabu hichi zimepigwa na mpiga picha maarufu Andrew Zuckerman zikiwa zinazonyesha bidhaa hizo za kampuni hiyo zilizotengenezwa miaka 20 iliyopita.
Zaidi ni kwamba Kitabu hicho kitaanza kuuzwa kupitia tovuti ya Apple.com hapo kesho, pia kitakuja na ukubwa tofauti ukubwa mdogo wa (smaller 10.20″ x 12.75″) pamoja na ukubwa mkubwa wa (larger 13″ x 16.25″), kitabu hicho kidogo kitauzwa dollar za marekani $199 = Tsh 440,000 na kikubwa kitauzwa kwa dollar za marekani $299 = Tsh 660,000. Ili kujua zaidi kuhusu kitabu hicho angalia video hapo chini.
Kama unataka kujua zaidi kuhusu kitabu hiki tembelea tovuti ya Apple.com na kwa habari zaidi za teknolojia enedlea kutembelea Tanzania tech kila siku au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.