Kampuni ya Apple hapo jana imetangaza kutoka kwa toleo lake jipya la mfumo wa iOS 11.3, Toleo hili jipya linakuja na sehemu mpya mbalimbali huku sehemu iliyo angaziwa sana ikiwa ni sehemu ya Battery. Kwa sasa unaweza kupakua toleo hilo kwenye simu yako ya iPhone au iPad na tegemea kukutana na maboresho haya.
- Battery Health (Beta) iPhone
Hii ni sehemu mpya ambayo itakuruhusu kuweza kuangalia ubora au uzima wa battery yako. Sehemu hii itakuwezesha kuangalia endepo battery yako inahitaji kubadilishwa au lah ikiwa pamoja na kuangalia uzima huo wa battery yako. Sehemu hii imekuja wakati watu wakilalamika kuwa kampuni ya Apple imekuwa ikifanya simu za zamani za Apple kupungua kasi na ubora wa battery.
Kutumia sehemu hii unaweza kuingia kwenye uwanja wa Settings > Battery > Battery Health (Beta) kisha angalia Maximum Capacity pamoja na maelezo ya Peak Performance Capability, hapo utaweza kuona kama simu yako inafanya kazi kwa kiasi kinachotakiwa sawa na siku ya kwanza kununua.
Kupata uhakika hakikisha Maximum Capacity unapata asilimia 100 na Peak Performance Capability unakuta maneno ya kukujulisha kuwa simu yako inafanya kazi kwa hali nayotakiwa.
- ARKit 1.5
Toleo jipya la iOS linakuja na sehemu mpya ya ARKit 1.5 ambayo hii itasaidia wabunifu mbalimbali wa programu kuweza kutengeneza programu zenye uwezo mzuri wa Augmented Reality. Sehemu hii pia inasaidia ramani kwenye mfumo huo kuweza kufanya kazi vizuri na kwa uhakika zaidi.
- Animoji Mpya (iPhone X)
Sehemu nyingine ambayo utegemee kukutana nayo ni aina mpya za Animoji ambazo hizi ni maalum kwa watumiaji wa iPhone X. Kama wewe ni mtumiaji wa simu hiyo basi ni vyema ukajua kuwa animoj mpya zilizo ongezwa ni pamoja na Animoji za simba, dubu, dragon na fuvu.
- iPad Charge Management (iPad)
Kwa upande wa iPad sehemu mpya iliyo ongezwa ni pamoja na sehemu mpya ya iPad charge management , sehemu hii itakuruhusu kuweza kufanya uangalizi wa battery yako hasa pale unapokuwa unachaji iPad yako kwa muda mrefu.
- Maboresho Mengine
Maboresho mengine ya mfumo wa iOS 11.3 ni madogo madogo ikiwa pamoja na maboresho ya keyboard, maboresho ya sera za faragha, maborsho ya kisakuzi cha Safari, maboresho ya App Store pamoja na maboresho mengine madogo madogo unaweza kusoma list nzima HAPA.
Kwa sasa unaweza kupakuwa mfumo huu mpya wa iOS 11.3 moja kwa moja kwenye kifaa chako kwa kuingia kwenye sehemu ya Settings > General > Software Update, hakikisha simu yako ni inayo bando ya kutosha kuanzia angalau GB 2 na kuendelea.
I love this website, Asante sana.
Karibu