Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Apple Kutoa iPad Mpya ya Inch 10.5 Mwezi April

Jiandae kwa ipad mpya kuanzia mwezi march mpaka mwezi april
ipad inch 10.5 ipad inch 10.5

Hivi karibuni kumekua na ripoti kadhaa kuhusu kuja kwa ipad mpya ya inch 10.5, hapo awali ripoti zilikua zinasema kuwa ipad hizo zingeanza kutengenezwa na kuingia sokoni kuanzia mwezi May au mwezi June mwaka huu 2017 lakini ripoti sasa zinasema kuwa wapenzi wa ipad kote duniani wategemee kuona ipad hizo kuanzia mwezi march mpaka april mwaka huu.

IPad hiyo inategemewa kutangazwa na kampuni ya Apple kwenye mkutano utakao fanyika mwezi April huko california. Vile vile ipad hiyo mpya ya inch 10.5 inakuja na kioo kikubwa ambacho kitakuwa kimejaa karibia ipad nzima hivyo itakuwa na (edge to edge display au bezel less) sehemu ambayo pia inategemewa kuja kwenye simu za iPhone 8 ambayo inatarajiwa kutoka baadae mwaka huu.

Advertisement

Ripoti hizo kutoka kwenye tovuti ya ditaltimes zinasema kuwa kampuni ya Apple pia inatarajia kuboresha matoleo yaliyopo ya ipad ya inch 9.7 pamoja na ile ya inch 12.9 ambazo pia zitatoka baadae mwaka huu. Kwa habari zaidi unaweza kutembelea tovuti ya digitaltimes kujua zaidi kuhusu tetesi na mambo yote yanaohusu ipad hiyo ya 10.5.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania tech kila siku pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari kwa haraka, pia usisahau kutufuata kwenye mitandao wa Youtube ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya Video.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use