Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Apple Inakuja na Kompyuta Mpya 3 za Mac Mwaka Huu

Jiandae na kompyuta mpya za Mac tatu mwaka huu zenye processor mpya
Kompyuta mpya za Mac Kompyuta mpya za Mac

Hivi karibuni ripoti kutoka kwenye tovuti ya Bloomberg zinasema kuwa, kampuni ya Apple iko kwenye hatua za awali za kumalizia kompyuta zake tatu ambazo zina tarajiwa kutoka mwaka huu 2018.

Habari hizo zinasema kuwa, Apple inategemea kuja na kompyuta hizo tatu ambazo mbili ni laptop au kompyuta mpakato na moja ni desktop au kompyuta ya mezani. Mbali na hayo kampuni ya Apple inatarajia kuleta kompyuta hizo mpya zikiwa na aina mpya ya processor ambazo zina tengenezwa na kampuni ya Apple yenyewe.

Advertisement

Hata hivyo hii sio ajabu sana kwa kampuni kama Apple kuamua kutengeneza processor za vifaa vyake yenyewe, tena hasa wakati huu ambapo bado kuna tahadhari ya virusi vya Spectre and Meltdown ambavyo hivi huathiri sana vifaa vina vyotumia processor za intel

Apple tayari inayo kompyuta ambazo zinatumia processor zake yenyewe kama vile kompyuta ya MacBook Pro ambayo inatumia ARM-based chip pamoja na kompyuta ya mezani ya iMac Pro.

Kwa sasa bado hakuna taarifa zaidi kuhusu lini kompyuta hizo mpya zitaingia sokoni, lakini tutaendelea kufuatilia habari hizi na tutakujulisha tutakapo pata taarifa zaidi.

Kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya Teknolojia, Pakua sasa App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia unaweza kujiunga na Channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili kujifunza mambo yote ya Teknolojia kwa njia ya video.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use