Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Apps za Kuangalia TV kwenye Simu ya Android (Hazipo Play Store)

Utaweza kuangalia channel za mpira wa miguu, filamu, burudani na makala
Apps za Kuangalia TV kwenye Simu ya Android (Hazipo Play Store) Apps za Kuangalia TV kwenye Simu ya Android (Hazipo Play Store)

Ni wazi kuwa hakuna mtu asiyependa kuangalia TV, lakini kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda kuangalia TV kwenye simu yako basi makala hii itakusaidia kuongeza njia mpya za kuangalia TV za kimataifa kwa urahisi kupitia kwenye simu yako ya Android.

Kupitia njia hii utaweza kuangalia channel mbalimbali za Michezo, Burudani, Filamu pamoja na channel zenye makala mbalimbali kwa lugha ya Kingereza. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie app hizi nzuri. Kumbuka Apps hizi hazipo Play Store hivyo pakua app hizi kupitia link chini ya maelezo ya app husika.

Advertisement

HD Streamz

Apps za Kuangalia TV kwenye Simu ya Android (Hazipo Play Store)

HD Streamz ni app ya android ambayo itakusaidia kungalia channel mbalimbali kutoka nje ya nchi, ikiwa pamoja na channel za michezo, burudani pamoja na channel nyingine mbalimbali. App hii inakuja na player maalum lakini ni vizuri kama ukitumia Mix Player kuweza kuangalia TV zilizopo ndani ya app hii. Unaweza kupakua app hii kupitia link hapo chini.

Download Hapa HD Streamz

Mobdro

Apps za Kuangalia TV kwenye Simu ya Android (Hazipo Play Store)

Mobdro ni app nyingine ambayo ni nzuri kwa wapenzi wa kuangalia TV kupitia simu ya Android, app hii inakuja na channel nyingi sana na ni rahisi sana kutumia. Kama wewe ni mpenzi wa michezo basi mobdro inakuja na kipengele maalum cha channel za michezo ambapo unaweza kupata michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu, mieleka, tenesi na michezo mingine mingi.

Download Hapa Mobdro

Cloud TV

Apps za Kuangalia TV kwenye Simu ya Android (Hazipo Play Store)

Cloud TV ni app nyingine ambayo itakusaidia sana kuangalia TV kwenye simu yako ya Android, ubora wa app hii unakuja hasa kwenye channel ya filamu pamoja na michezo. Kupitia app hii utaweza kuona channel nyingi sana za michezo huku channel nyingi zikiwa zinaonyesha michezo ya mpira wa miguu pamoja na michezo mingine mbalimbali.

Download Hapa Cloud TV

VIU Premium

Apps za Kuangalia TV kwenye Simu ya Android (Hazipo Play Store)

App ya mwisho kwenye list hii ni tofauti na nyingine, kama wewe ni mpenzi wa tamthilia mbalimbali kama india, Nigeria, Kenya, Korea, Ghana, Pakistani na nchi nyingine basi app hii itakufaa sana. App hii inakuja na filamu nyingi pamoja na tamthilia ambazo unaweza kuangalia ndani ya app hii moja kwa moja au kwa kudownload moja kwa moja kupitia kwenye app hiyo.

Download Hapa VIU Premium

Na hizo ndio app nzuri za kuangalia TV ambazo hazipatikani kwenye soko la Play Store, kama unataka kujua app nyingine nzuri, unaweza kusoma hapa kujua app za kutuma SMS nyingi kwa pamoja kwenda kwa wateja wako au familia kwa urahisi na haraka.

Kufahamu app nyingine nzuri hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku, pia hakikisha unajiunga na channel ya Tanzania Tech kupitia mtandao wa YouTube Hapa.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use