Kampuni ya Microsoft’s tayari imesha anza mkutano wake wa Build developer conference ambao hufanyika na kampuni hiyo kila mwaka, ndani ya mkutano huo kampuni ya Microsoft huonyesha baadhi ya mambo yanayotegemewa kuja kwenye mfumo wake wa uendeshaji wa Windows 10 pamoja na bidhaa nyingine kutoka kampuni hiyo.
Mwaka huu moja ya maboresho ya Windows 10 yanayo tarajiwa ni pamoja na programu mpya kabisa inayo itwa “Your Phone”. Programu hii itakuwezesha kutumia simu yako yenye mfumo wa Android au iOS moja kwa moja kwenye kompyuta yako inayotumia mfumo wa Windows 10.
Hata hivyo kwa mujibu tovuti ya Engadget, programu hiyo itakuwa inafanya kazi vizuri zaidi kwenye simu za Android kuliko kwenye mfumo wa iOS, kwani kwenye mfumo huo utakuwa na uwezo wa kuamisha data kati ya kivinjari cha kompyuta yako na kivinjari cha simu, na ili kufanya hivyo nilazima uwe umepakua kivinjari cha Microsoft’s Edge browser kwenye simu yako ya mfumo wa iOS na pia lazima uwe unatumia kivinjari hicho kwenye kompyuta yako yenye mfumo wa Windows 10.
Kwa upande wa watumiaji wa Android, utaweza kusoma meseji zako zilizoko kwenye simu yako kwa kutumia kompyuta, pia utaweza kuona taarifa za ujumbe mfupi (notification) kutoka kwenye simu yako. Vilevile utaweza kutumia picha kwa urahisi kati ya simu yako na kompyuta yako yenye mfuno wa Windows 10.
Microsoft imetangaza kuwa, sehemu hii inatarajia kuja kwanza kwa watumiaji wa mfumo wa Windows 10 wa majaribio unao julikana kama Windows Insider Program, na baadae programu hiyo itakuja kwa watumiaji wengie wote wa kompyuta zenye mfumo wa Windows 10.
Hata hivyo kwa sasa bado haijajulikana kama programu hiyo ya Your Phone itakuja kama programu ya kujitegemea kutoka Microsoft au kama sehemu ya sasisho jipya la mfumo wa Windows 10, endelea kutembelea Tanzania Tech kujua zaidi.