WHO Yatangaza Ujio wa Apps Mpya Kwaajii ya COVID-19

Sasa utaweza kupata taarifa kwa urahisi kutoka WHO kwenye simu yako
WHO Yatangaza Ujio wa Apps Mpya Kwaajii ya COVID-19 WHO Yatangaza Ujio wa Apps Mpya Kwaajii ya COVID-19

Wakati dunia ikiendelea na mapambano dhidi ya virusi vya corona, shirika la Afya duniani WHO lime endelea kuangalia njia nyingine mpya za kufikisha habari na elimu kwa jamii kwa kutumia teknolojia.

Kwa mujibu wa tovuti ya 9to5google, hivi karibuni WHO imetangaza kuja na apps zake za Android pamoja na iOS ambazo zitasaidia kufikisha ujumbe kwa jamii kwa haraka ikiwa pamoja na kutoa elimu dhidi ya virusi vya corona au COVID-19. App hizo ambazo zimepewa jina la WHO COVID-19 kwa sasa zipo kwenye hatua za majaribio na tayari zimepakuliwa kwa mara zaidi ya 1000 kupitia kwenye soko la Play Store.

Advertisement

WHO Yatangaza Ujio wa Apps Mpya Kwaajii ya COVID-19

Kwa upande wa app ya Android ambayo hadi sasa ndio inapatikana kwenye soko la Play Store ikiwa kwenye majaribio. App hiyo inaonyesha taarifa mbalimbali za muhimu ikiwa pamoja na jinsi ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona, nadharia ambazo sio za ukweli kuhusu virusi vya corona pamoja na taarifa mbalimbali juu ya jinsi ya kujilinda pamoja na habari mbalimbali kuhusu maambukizi kwa dunia nzima hadi sasa.

WHO Yatangaza Ujio wa Apps Mpya Kwaajii ya COVID-19

Kwa sasa inasemekana kuwa bado app hii ya Android pamoja na iOS zipo kwenye hatua za awali za majaribio, na zitaendelea kuongezewa baadhi ya sehemu nyingine za muhimu ambazo zitasaidia watumiaji kujua namna mbalimbali za kuzuia maambukizi ikiwa pamoja na kutoa msaada kwa wahudumu wa afya kujua zaidi kuhusu mtu yoyote ambaye tayari amesha ambukizwa.

Kama unataka kujaribu App hii kwa sasa inapatikana kwa watumiaji wa Android na unaweza kupakua app hii ikiwa kwenye hatua ya majaribio kupitia link hapo chini.

WHO COVID-19 Updates
Price: To be announced

Kwa watumiaji wa iOS app hii iatarajiwa kuzinduliwa siku za karibuni hivyo endelea kutembelea ukurasa huu tutaongeza app hiyo pale itakapo zinduliwa rasmi.

Kupata taarifa zaidi kuhusu virusi vya corona ukiwa hapa nchini Tanzania hakikisha unatembelea tovuti ya wizara ya Afya, pia unaweza kusikiliza vyombo vya habari vinavyo aminika hapa nchini kwa ajili ya kupata taarifa zilizo sahihi na zilizo thibitishwa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use