Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

App Mpya ya Tanzania Tech kwa Watumiaji wa Apple Mfumo wa iOS

Sasa utaweza kusoma makala mpya za Tanzania Tech kupitia App ya iOS
App ya iOS Tanzania Tech (1) App ya iOS Tanzania Tech (1)

Habari ya muda huu msomaji wetu, ni muda mrefu umepita toka tuandike habari inayo tuhusu sisi na leo ningependa angalau kwa sasa nikujuze mambo ya msingi kuhusu sisi pamoja na tovuti ya Tanzania Tech kwa ujumla.

Kwanza napenda kuchukua nafasi hii, kutoa shukurani zangu kwa niaba ya timu nzima ya Tanzania Tech, kwani mwaka jana 2017 ulikua ni mwaka mzuri sana na tumeweza kufanya mambo mengi sana mazuri kwa kushirikiana na wewe msomaji wetu. Bado tuna mipango mingi sana ya kuboresha weledi pamoja na kuboresha huduma zetu kwa ujumla, hivyo bado tunaomba support yako kwa kuendeleza ushirikiano wako na sisi.

Advertisement

Najua ni weekend hivyo sinto-kuchosha sana na maneno mengi bali nitaenda moja kwa moja kwenye nia ya makala hii. Hapa kuna jambo ambalo ningependelea ufahamu wewe kama msomaji wetu mpendwa na jambo lenyewe ni kuhusu ujio wa App ya Tanzania Tech kwa wasomaji wetu wanaotumia mfumo wa iOS.

Kwa sasa App yetu ya Tanzania Tech kwa mfumo wa iOS ipo kwenye hatua za mwisho kabisa na ina fanyiwa ukaguzi na wataalamu wetu ikiwa pamoja na kuangalia matatizo mbalimbali yanayojitokeza kwenye hatua hii ya hawali. Kwa sasa napenda kushiriki na nyie muonekano wa App hiyo ambayo itanza kupatikana siku za karibuni.

App hii kwa sasa imekamilika lakini bado ipo kwenye hatua za majaribio na siku za karibuni wote mnao tumia mfumo wa iOS mtaweza kuipakua kupitia soko la App Store. Kwa sasa unaweza kuanza kujaribu toleo la awali kwa kudownload App ya Test Fight kupitia App store kisha andika kwenye sehemu ya maoni “nataka kujaribu app” nasi tutakutumia code ambazo zita kuwezesha kupakua App hiyo na kujaribu kwenye simu yako kabla ya kutoka rasmi.

‎TestFlight
Price: Free

Tuna tegemea kuendelea kufanya maboresho zaidi kwenye App hii pamoja na kuongezea vitu vingi zaidi ambavyo vitafanya App hiyo iwe rahisi kutumia na bora zaidi. Na kwa watumia wa app ya Android pia vilevile tunategemea kufanya maboresho zaidi pamoja na kuongeza sehemu mpya.

Kwa leo nadhani niishie hapo na kwa mara nyingine, ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa niaba ya wafanyakazi wa Tanzania Tech kwa ujumla na tunapenda kuendelea kupata support yako kwa kutembelea tovuti yetu pamoja na huduma zetu nyingine kila siku. Asanteni Sana..!!

6 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use