App ya Instagram Yaongezewa Aina Mpya ya Stika za Kupiga Kura

Mtandao wa Instagram waleta stika mpya za Poll
Instagram Poll Instagram Poll

Mtandao wa instagram unaendelea kukua kila siku hivi karibuni mtandao huo ulifikisha watumiaji zaidi ya milioni 800 kwa mwezi huku ikiwa na rekodi ya watumiaji zaidi ya milioni 500 wanaotumia mtandao huo kila siku, pengine ukuaji huu ndio unaofanya Instagram kuleta sehemu mpya kwenye app zake ili kuvutia watu wengi zaidi.

Hivi karibuni mtandao huo umeleta aina mpya ya stika kwenye programu zake za Android pamoja na iOS ambazo stika hizo zinakupa uwezo wa kupiga kura mbalimbali kupitia sehemu ya “Stories na Live Video”.

Advertisement

Unachotakiwa kufanya wakati unachukua bofya sehemu ya “Stories” kisha chagua picha au ingia kwenye Live Video kisha bofya kwenye sehemu ya “Sticker” kisha chagua stika iliyo andikwa “POLL” kisha andika swali lenye majibu mawili unayotaka watu wanao angalia wachague na utaweza kuona matokeo ya maswali yako moja kwa moja kwenye app ya Instagram.

Sehemu hii kwa mara ya kwanza ilionekana kwenye App za Snapchat na ni wazi kuwa Instagram ime endelea kuchukua baadhi ya sehemu kwenye mtandao wa Snapchat na kuziboresha zaidi au kubadilisha kidogo, picha hapo chini ni sehemu hiyo mpya kwenye instagram pamoja na snapchat.

Kujua zaidi kuhusu mitandao hii endelea kutembelea Tanzania Tech nasi tutakujuza yote mapya, pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka zaidi.

Chanzo : Instagram Blog

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use