Sera ya Faragha Maelezo yafuatayo yanaelezea sera yetu ya faragha kuhusiana na taarifa za mtu za kibinafsi ambazo tunakusanya kuhusiana na wewe.
TABLE OF CONTENTS
- 1 Maelezo ya Dhamira
- 2 Taarifa za Wageni
- 3 Cookie ni nini?
- 4 Matumizi na Hifadhi ya Taarifa Zako za Kibinafsi
- 5 Kupata Taarifa Zako za Kibinafsi
- 6 Watumiaji Wenye Umri wa Miaka 16 au Pungufu
- 7 Jinsi ya Kutafuta na Kudhibiti Cookies Zako
- 8 Utajuaje Kurasa Gani Ulizopitia Zinatumia Cookies?
- 9 Jinsi ya Kuangalia Alama ya Cookie Yako
- 10 Udhibiti wa Jumla na Ulinzi wa Data (GDPR)
- 11 Hitimisho
Maelezo ya Dhamira
Mara kwa mara, utaombwa kuwasilisha taarifa zako za kibinafsi (kwa mfano, jina na anuani ya email, nk) ili kupata au kutumia huduma zilizopo kwenye mtandao wetu. Huduma hizo ni pamoja na vijarida, mashindano, “Batilisha Email”, mazungumzo ya moja kwa moja, ubao wa ujumbe na uanachama wa Tanzania Tech.
Kwa kuandika maelezo yako kwenye nafasi zilizopo, unairuhusu Tanzania Tech na mashirika yake yanayotoa huduma kukupatia huduma ulizoziomba. Kila unapotoa maelezo yako ya kibinafsi, tutahifadhi taarifa hizo kwa kuzingatia sera hii. Huduma zetu zimekusudiwa kukupatia taarifa unazotaka kupata. Tanzania Tech itashughulika kulingana na sheria za sasa hivi na itadhamiria kutekeleza taratibu nzuri kabisa za sasa hivi za Internet.
Taarifa za Wageni
Wakati wowote unapotembelea mtandao wa Tanzania Tech, kurasa unazoziona, pamoja na kitu kinachoitwa cookie, zinaingizwa kwenye kompyuta yako (angalia kipengee cha 3 kupata mengi juu ya hili). Karibu kurasa zote, kama siyo zote kabisa, zinafanya hivyo, kwa sababu cookies zinaiwezesha kampuni inayomiliki kurasa hizo kufanya vitu vingi vyenye manufaa, kama vile kujua kama kompyuta hiyo (na huenda mtumiaji wake) ametembelea ukurasa huo hapo awali. Hii inafanyika wakati mtumiaji huyo anarejea tena kwenye mtandao, kwa kuchunguza ili kuangalia na kuikuta cookie iliyoachwa hapo nyuma, wakati mtumiaji alipozuru mtandao mara ya mwisho.
Taarifa yoyote ambayo imetolewa na cookies inaweza kutusaidia kukupa wewe huduma bora na kutusaidia kuchunguza wasifa wa wageni wetu. Kwa mfano: kama ulipotembelea kurasa zetu mara ya mwisho, tuseme uliingia kwenye kurasa za maujanja, basi tunaweza kukuta taarifa hizi kwenye cookie yako na kielelezo cha taarifa za maujanja utakapoingia mara ya pili
Cookies hizo na alama iliyopo kwenye mtandao vinatoa takwimu ambazo siyo za kibinafsi kuhusu ziara zilizofanywa kwenye kurasa zetu, muda uliotumika kuangalia ukurasa, njia zilizotumiwa na wageni hao kwenye mtandao, data zilizopo kwenye mipangilio ya skrini za wageni na taarifa nyingine za kawaida. Tanzania Tech inatumia taarifa kama hizi, na zile zilizopatikana kwenye cookies nyingine zilizotumika kwenye mtandao huo kusaidia kuboresha huduma kwa watumiaji wake.
Kama unataka kuikataa cookie unaweza kushindwa kutumia mtandao wetu vizuri na unaweza kutumia utaratibu uliowekwa hapo chini katika kipengee cha 7. Kuilemaza (kuiondoa) alama iliyowekwa kwenye mtandao, unapaswa kupeleka maombi yako moja kwa moja kwa privacy@tanzaniatech.one.
Cookie ni nini?
Unapoingia kwenye mtandao kompyuta yako mara moja itapewa cookie. Cookies ni faili za maandishi zinazoitambulisha kompyuta yako kwa mtambo wetu wa mtandao unaohifahdi kumbukumbu zote (server). Cookies zenyewe hazimtambui mtumiaji, ila tu zinaitambua kompyuta iliyotumiwa. Makampuni mengi ya mtandao yanafanya hivyo wakati mtumiaji anapozuru kurasa zao ili kuweza kujua jinsi watu wanavyoingia na kutoka kwenye mtandao huo.
Cookies zeneywe zinachukua kumbukumbu za maeneo ya mtandao ambayo yametembelewa na kompyuta husika, na kwa muda gani. Watumiaji wanapata fursa ya kuzifanya kompyuta kuruhusu cookies zote, kuwafahamisha wakati ambapo cookie imetolewa, au kutopokea cookies wakati wowote ule. Hilila mwisho linamaanisha kwamba huduma fulani fulani za kibinafsi hazitaweza kutolewa kwa mtumiaji huyo.
Matumizi na Hifadhi ya Taarifa Zako za Kibinafsi
Unapotoa taarifa zozote za kibinafsi kwa Tanzania Tech (kwa mfano, kwa ajili ya mashindano, huduma za jamii za Tanzania Tech (Tanzania Tech Community) au uanachama wa Tanzania Tech kisheria tunawajibika kwako katika kuangalia jinsi tunavyotumia data hizo.
Tunapaswa kukusanya taarifa hizo kwa haki, hii inamaanisha kwamba tunalazimika kukuelezea jinsi tutakavyo tumia data hizo (angalia matangazo kwenye kurasa husika ambazo zinakufahamisha kwa nini tunaomba maelezo hayo) na kukuambia kama tunataka upeleke taarifa hizo kwa mtu mwingine yeyote yule. Kwa kawaida, taarifa zozote zile unazozitoa kwa Tanzania Tech zitatumika ndani ya Tanzania Tech na watu wake wanaotoa huduma. Kamwe hazitapelekwa kwa mtu yeyote yule nje ya Tanzania Tech bila kupata idhini yako kwanza, isipokuwa tunapo wajibika au tunaporuhusiwa kisheria kufichua taarifa hizo.
Vile vile, kama unatuma au kupeleka maelezo yenye matusi au yasiyofaa juu ya Tanzania Tech au kwa Tanzania Tech Media itaona kwamba mwenendo huo ni mbaya na/au umerudiwa, Tanzania Tech inaweza kutumia taarifa zozote zile zilizopatikana kuhusiana na wewe ili kukomesha mwenendo huo. Hii ni pamoja na kuwafahamisha watu wengine kama vile mwajiri wako, shule yako au kampuni inayotoa huduma za barua-pepe kuhusu yaliyomo kwenye maandishi yako au juu ya mwenendo wako.
Tutahifadhi taarifa zako za kibinafsi katika mitambo yetu katika muda wote ule ambao unatumia huduma yetu uliyoiomba, na tunaweza kuziondoa wakati lengo litakapotekelezwa, ama kwa upande wa uanachama wa Tanzania Tech utakapoamua kwamba hutaki tena kuendeleza usajili wako kama mwanachama wa Tanzania Tech. Hata hivyo kwa sababu za kiusalama,Tanzania Tech inaweza kuhifadhi data za maandishi ya ujumbe (ikiwa ni pamoja na yaliyomo kwenye ujumbe, majina na wanachama, muda na tarehe) zilizotokana na matumizi ya huduma za jamii za Tanzania Tech (Tanzania Tech Community) kama vile Connector kwa muda wa miezi sita. Mahali ambako taarifa za kibinafsi zimehifadhiwa kwa ajili ya watu ambao bado hawajasajiliwa, lakini wameshiriki katika huduma nyingine za Tanzania Tech (kwa mfano vile mashindano), taarifa hizo zitahifahdiwa kwa kipindi kitakacho onekana kwamba kinafaa ili kuhakikisha kwamba huduma hizo zinaendeshwa vizuri. Tutahakikisha kwamba taarifa za kibinafsi zilizotolewa zinahifadhiwa vizuri katika hali ya usalama, kulingana na Sheria ya Kulinda Data ya mwaka 1998 (Data Protection Act 1998).
Kama umearifiwa kwenye mtandao wa Tanzania Tech kwamba taarifa zako zinaweza kutumiwa kuiwezesha Tanzania Tech kuwasiliana na wewe kwa ajili ya “huduma za kiutawala”, hii inamaanisha kwamba Tanzania Tech inaweza kuwasiliana na wewe kwa sababu kadhaa zinazohusiana na huduma uliyojiandikisha nayo. Kwa mfano, tunaweza kukupatia huduma ya habari kwa barua pepe yako au kukujulisha kwamba huduma husika imesimamishwa kwa matengenezo. Hatutawasiliana na wewe kwa ajili ya kutoa matangazo, kama vile kukujulisha juu ya kuboresha huduma zetu au juu ya vipindi vipya vya Tanzania Tech, isipokuwa kama unakubali bayana kwamba tuwasiliane nawe kwa malengo kama hayo wakati unapowasilisha taarifa zako kwenye mtandao, au baadaye kama utajiandikisha kwa madhumuni mahsusi ya kupokea taarifa kama hizo za matangazo.
Kupata Taarifa Zako za Kibinafsi
Una haki ya kuomba nakala ya taarifa zako za kibinafsi zinazokuhusu ambazo Tanzania Tech inazihifadhi na kusahihisha maelezo yoyote yenye makosa. (Huduma hizo zinapatikana kupitia App zetu au kama unatuma maoni kwenye tovuti yetu na huduma nyingine za Tanzania Tech).
Watumiaji Wenye Umri wa Miaka 16 au Pungufu
Kama una umri wa miaka 16 au miaka pungufu ya hapo, tafadhali pata idhini kutoka kwa mzazi/mlezi wako wakati wote unapotaka kutoa maelezo yako ya kwenye mtandao wa Tanzania Tech. Watumiaji ambao hawana idhini ya aina hiyo hawaruhusiwi kutupatia taarifa zao za kibinafsi au kutumia mtandao wa Tanzania Tech kwa ujumla.
Jinsi ya Kutafuta na Kudhibiti Cookies Zako
Kama unatumia Google Chrome : Kwenye Task Bar, bonyeza: 1. Settings, kisha 2. bonyeza Content 3. Bonyeza Hatua ya Juu Cookies 4. Bonyeza Allow sites to save and read cookie data (recommended) unaweza kuzima Cookies hapo.
Kama unatumia Internet Explorer 6.0: 1. Chagua Vifaa (Tools) 2. Chaguo la Internet (Internet Options) 3. Bonyeza kitufe cha Faragha (Privacy Tab) 4. Bonyeza Kiwango cha Mteja (Custom Level) 5. Bonyeza kitufe cha Hatua ya Juu (‘Advanced’) 6. Chunguza kishubaka cha ‘override automatic cookie handing’ na chagua Kubali (Accept), Zuia (Block) au Chochea (Prompt) kwa ajili ya utekelezaji wa hatua inayofaa.
Kama unatumia Internet Explorer 5.0 or 5.5: 1. Chagua Vifaa (Tools), kisha 2. Chaguo la Internet (Internet Options) 3. Bonyeza kitufe cha Usalama (Security tab) 4. Bonyeza Kiwango cha Mteja (Custom Level) 5. Nenda chini katika chaguo la sita kuangalia jinsi cookies zinavyodhibitiwa na IE5 na badilisha uende Kubali (Accept), Lemaza (Disable), au Chochea (Prompt) kwa ajili ya utekelezaji wa hatua inayofaa.
Kama unatumia Internet Explorer 4.0: 1. Chagua Angalia (View), kisha 2. Chaguo la Internet (Internet Options) 3. Bonyeza kitufe cha Hatua ya Juu (Advanced) 4. Nenda chini kwenye alama ya mshangao chini ya Usalama (Security) na uchague mojawapo kati ya haya mambo matatu ili kusawazisha matumizi yako ya cookies.
Katika Internet Explorer 3.0: Unaweza Kuangalia (View), Kuchagua (Options), na kwenda Hatua ya Juu (Advanced), kasha bonyeza kwenye kitufe kinachosema Onyo (Warn) kabla ya Kukubali (Accepting) Cookies.
Utajuaje Kurasa Gani Ulizopitia Zinatumia Cookies?
Kama unatumia Google Chrome : Kwenye Task Bar, bonyeza: 1. Settings, kisha 2. bonyeza Content 3. Bonyeza Hatua ya Juu Cookies 4. Bonyeza See all cookies and site data hapo unaweza kuona kurasa zote zinazo tumia Cookies.
Kama unatumia Internet Explorer 5.0 or 6.0: 1. Chagua Tools, kisha 2. Chaguo la Internet (Internet Options) 3. Click the General tab 4. Bonyeza Mipangilio (Settings) 5. Angalia Faili (View Files)
Kama unatumia Internet Explorer 4.0: Kwenye Task Bar yako, bonyeza: 1. Angalia (View), kisha 2. Chaguo la Internet (internet Options) 3. Chini ya nembo General (the default tab) bonyeza 4. Mipangilio (Settings) 5. Angalia Faili (View Files)
Internet Explorer 3.0: Kwenye Task Bar yako, bonyeza: 1. Angalia (View) 2. Chaguo (Options) 3. Hatua ya Juu (Advanced) 4. Angalia Faili (View Files)
Jinsi ya Kuangalia Alama ya Cookie Yako
Bonyeza kwenye cookie ili kuifungua. Utaona mstari mfupi wa maandishi na tarakimu. Tarakimu hizo ni kadi ya kitambulisho chako, ambacho kinaweza kuonekana na kampuni iliyokupa cookie hiyo.
Udhibiti wa Jumla na Ulinzi wa Data (GDPR)
Sisi ni Mdhibiti wa baadhi ya data na maelezo yako.
Msingi wa kisheria wa Tanzania Tech Media wa kukusanya na kutumia taarifa za kibinafsi zilizofafanuliwa katika Sera hii ya Faragha unategemea Taarifa za Kibinafsi tunazokusanya na muktadha mahususi ambamo tunakusanya taarifa:
Tanzania Tech Media inahitaji kufanya mkataba na wewe
- Umeipa Tanzania Tech Media ruhusa kufanya hivyo
- Kuchakata taarifa zako za kibinafsi ni kwa maslahi halali ya Tanzania Tech Media
- Tanzania Tech Media inahitaji kuzingatia sheria
- Tanzania Tech Media itahifadhi taarifa zako za kibinafsi kwa muda tu inavyohitajika kwa madhumuni yaliyoainishwa katika Sera hii ya Faragha. Tutahifadhi na kutumia maelezo yako kwa kiwango kinachohitajika ili kutii majukumu yetu ya kisheria, kutatua mizozo na kutekeleza sera zetu.
Ikiwa wewe ni mkazi wa Eneo la Kiuchumi la Ulaya (EEA), una haki fulani za ulinzi wa data. Iwapo ungependa kufahamishwa ni Taarifa gani za Kibinafsi tunazoshikilia kukuhusu na ukitaka ziondolewe kwenye mifumo yetu, tafadhali wasiliana nasi.
Katika hali fulani, una haki zifuatazo za ulinzi wa data:
- Haki ya kufikia, kusasisha au kufuta maelezo tuliyo nayo juu yako.
- Haki ya kurekebisha.
- Haki ya kupinga.
- Haki ya kizuizi.
- Haki ya kubebeka kwa data
- Haki ya kuondoa kibali
Hitimisho
Kama una maswali au maoni yoyote kuhusu sera hizi za faragha unaweza kuwasiliana nasi kwa kutumia fomu ya wasiliana nasi inayopatikana chini au mwisho wa tovuti hii.
Sera hizi za Faragha zime haririwa rasmi Tarehe 24/03/2022
— Mabadiliko Hivi Karibuni —
Tumeongeza Udhibiti wa Jumla na Ulinzi wa Data (GDPR)