Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Apps #16 App Nzuri za Kuedit Video Kwenye Simu ya Mkononi

App hizi zitakusaidia kutengeneza video zako kwa namna ya kipekee
App za Kuedit Video App za Kuedit Video

Hivi karibuni instagram imezindua IGTV, sehemu maalum kwaajili ya video ndefu kupitia mtandao wa Instagram. Pamoja na kuja kwa sehemu hii bado changamoto imekuwa ni jinsi ya kutengeneza video hizi na jinsi ya kuedit video hizo kupitia simu ya mkononi.

Tanzania Tech tumeliona hilo na leo tunakuletea App nzuri za kuedit video kupitia simu yako ya mkononi. App hizi ni nzuri na ni rahisi sana kutumia na zitakusaidia sana kuedit video zako kwa haraka na kwa kutumia simu yako ya mkononi. Baadhi ya App hizi zinapatikana kwenye mifumo yote ya iOS pamoja na Android, basi bila kupoteza muda twende tukangalie app hizi nzuri.

Advertisement

1. Antix – Video Editor inc GoPro

  • Android
  • iOS
‎Antix Video Editor
Price: Free

Antix ni moja kati ya app nzuri sana kwaajili ya kuedit video kupitia simu yako ya mkononi, App hii haina matangazo haina sehemu ya kufanya manunuzi, app hii ni ya bure kabisa na inauwezo wa kuediti video kwa njia ya kisasa kabisa kwaajili ya kutuma kwenye mitandao ya kijamii kama instagram, Facebook na Youtube.

2. KineMaster

  • Android
  • iOS
‎KineMaster (OLD)
Price: Free+

KineMaster ni moja kati ya App za zamani na bora kwaajili ya kuedit video kupitia kwenye simu yako ya Android au iOS. Kama unataka muonekano wa pekee kwenye video zako unazotuma kwenye mitandao ya kijamii basi nakushauri ujaribu programu hii ya KineMaster.

3. PowerDirector Video Editor App – Android

Kama simu yako inayo teknolojia ya 4K au hata kama haina na ungependelea kutengeneza video zenye teknolojia hiyo kupitia simu yako ya mkononi basi pakua app hii ya PowerDirector. App hii ni nzuri sana kwa wale wanaopenda video zao kuonekana vizuri na bora zaidi, app hii ni moja kati ya app chache zenye uwezo wa kuweka slow motion kwenye video zako, miongoni mwa mambo mengine mengi. Kama unataka utofauti kwenye video zako, pakua sasa app hii.

4. ActionDirector Video Editor – Edit Videos Fast

ActionDirector Video Editor ni app nzuri sana kwa kuedit video kwa haraka, app hii inarahisha sana kazi ya kuediti picha kwa wale watu ambao hawataki kupoteza muda mwingi. App hii ni rahisi kutumia na inaweza kutengeneza video kwaajili ya mitandao mbalimbali ya kijamii.

5. FilmoraGo – Free Video Editor

  • Android
  • iOS

FilmoraGo ni app nyingine nzuri ya kuedit video, tofauti na app nyingine kwenye list hii app ya FilmoraGo itakusaidia kuweka vikorombezo (Effect) kwenye video zako kwa haraka sana. App hii inapatikana kwenye mifumo ya Android na iOS.

Na hizo ndio app nzuri nilizokuandalia leo kwaajili ya kuedit video, kama kuna app nyingine unayo ijua yenye uwezo mzuri wa kuedit video kwenye simu, basi unaweza kutuandikia kwenye sehemu ya maoni hapo chini. Vilevile kama ulipitwa na App nyingine nzuri za kuangalia kombe la dunia unaweza kujaribu app hizo kwenye simu yako kwa kusoma hapa.

4 comments
  1. Mimi nataka kujua jinsi ya kupunguza sauti ya muvi wakati wa kutafsili. Yani ninapo tafsili Mimi nataka sauti ya muvi iwe chini Niki nyamaza ya muvi ipande je ni fanyeje?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use