Moja kati ya jambo ambalo ni gumu sana kwa sasa ni hili la kushindwa au kuchelewa kupata baadhi ya huduma kutokana na janga la virusi vya corona. Hii inatokana na watu mbalimbali kufanyia kazi nyumbani na hivyo kuchelewa au kushindwa kufikisha huduma kwa wateja kwa urahis kama ilivyokuwa awali.
Kupitia makala hii nitaenda kutaja baadhi ya app au programu ambazo zitakusaidia kufanya kazi kwa urahisi na haraka ukiwa nyumbani. Kumbuka list hii ni mchanganyiko wa app mbalimbali hivyo hakikisha unasoma makala hii hadi mwisho kuweza kujua app ambazo zinaweza kukusaidia zaidi.
TABLE OF CONTENTS
Zoom
Zoom ni moja ya app ambayo kwa sasa imepata umaarufu mkubwa lakini pia imepata sifa mbaya kwa baadhi ya nchi kwa kusemekana kuwa sio salama kwa asilimia 100. Lakini kutokana na uwezo wake wa kufanya kazi hii ni moja kati ya app ambayo ni muhimu sana kuwa nayo kwani inakusaidia kuwasilina na wafanyakazi wenzako kwa pamoja ikiwa pamoja na kutumiana mafaili na kushare screen yako kwa urahisi sana. Kama unashindwa kupakua app hii kwa link hapo unaweza kujaribu kupitia link.
Microsoft Teams
Microsoft Team ni app nyingine nzuri ambayo unaweza kutumia kufanya kazi nyumbani, app hii kama iliyopita hapo juu nayo inakuja na uwezo wa kukusaidia kuchat na watu mbalimbali ikiwa pamoja na kupiga simu za pamoja za sauti pamoja na simu za Video.
Microsoft Office: Word, Excel, PowerPoint & More
Kupitia app hii utaweza kufungua mafle yote unayo tumiwa kupitia simu yako, utaweza kufungua mafile ya Office, Power Point, Excel na PDF. App hii ni nzuri sana na ni moja kati ya app ambayo nadhani kila mtu anahitaji kuwa nayo kwenye simu yako sasa.
My Price List – Simple and Easy Price List Maker
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanafanya biashara na wateja wanahitaji uwatumie bei za bidhaa zako basi app ya My Price List ni ya muhimu kwako kwani app hii inaweza kukusaidia kutengeneza price list na kuwatumia wateja wako kwa urahisi kabisa.
Invoice Maker: Estimate & Invoice App
Invoice Maker ni app nyingine nzuri ambayo inakusaidia kuandaa ankara ya malipo kwa wateja wako, app hii ni nzuri sana na ni rahisi kutumia hivyo huna haja ya kuwa na utaalamu wowote ili kuweza kutumia. Pia utaweza kupata taarifa pale mtu atakapo weza kuangalia ankara uliyo mtumia.
WhatsApp Business
Mpaka sasa nadhani karibia kila mtu anatumia au anaijua app ya WhatsApp business, mbali ya kuwa hii ni app kama ilivyo app ya WhatsApp, lakini hii inakuja na sehemu nyingine nyingi kwaajili ya wafanya biashara. Kupitia app ya WhatsApp Business utaweza kutuma picha za bidhaa zako zikiwa pamoja na bei zake kwa weteja wako kwa urahisi na haraka kupitia sehemu ya Catalog.
Goby
Goby ni app nyingine ambayo inaleta urahiwa wa kufanya kazi nyumbani, app hii inakuruhusu kutengeneza soko la mtandaoni na moja kwa moja utaweza kupokea malipo kwa tigo pesa na Mpesa pale mtu atakapoweza kununua bidhaa yako. Kupitia app hii utapata link maalum ambayo hiyo itakusaidia kuweza kushare na watu ili waweze kuona bidhaa zako bila hata kuwa na app hii. App hii inachaji gharama kuanzia Tsh 1000 na kuendelea.
Brochure Maker
Kama wewe ni mtu wa masoko basi kwa sasa ni kupindi ambacho ni lazima kuamia kufanya mambo kidigital, hii inahusisha kutengeneza matangazo ya online na mambo mengine mengi. Lakini kama utakuwa unao uhitaji wa kutengeneza Brochure basi app hii itakusaidia sana kuweza kufanya hivyo. Kupitia app hii utaweza kutengeneza Brochure za kisasa ambazo unaweza kushare na wateja.
Ad Maker, Banner Maker For Digital Marketing
Kwa sasa kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanatafuta masoko kupitia mtandao wa instagram basi najua ni lazima unakutana na changamoto ya kutengeneza matangazo bora ambayo yatavutia wateja wako. Kupitia app hii ya Ad Maker utaweza kutengeneza matangazo bora na rahisi kwaajili ya Instagram ambayo yatakusaidia kuvuta wateja zaidi.
Ad Maker, Video Editor, Explainer Video Maker
Kama unataka kutengeneza matangazo ya instagram au mitandao mingine kwa kutumia video basi app hii ya Ad Maker ni app nyingine ambayo ni nzuri sana kwako. App hii inakuja na uwezo wa kutengeneza video kwa haraka na unaweza kutengeneza bila kuwa na ujuzi wowote wa ku-edit video kwa namna yoyote.
Na hizo ndio baadhi tu ya app ambazo zinaweza kukusaidia kufanya kazi ukiwa nyumbani kwa urahisi kama unataka kujua app nyingine nzuri ambazo unaweza kujaribu kwenye simu yako ya Android basi unaweza kusoma hapa kujua app nzuri za ambazo zinaweza kukusaidia kutambua jina la nyimbo yoyote kwa urahisi na haraka.
Abali, naomba kusaidiwa app inayo weza kuniingizia kipato kupitia Internet tu pasipo biashara msaada