Ni kweli kuwa simu hasa za mfumo wa Android zina uwezo wa kufanya mambo mengi sana, lakini mambo hayo mengi hayawezekani mpaka kuwa na apps ambazo zinaweza kukusaidia kufanya mambo hayo kwa urahisi, kuliona hili leo nimekuletea sehemu ya 2 ya App nzuri za Android ambazo unaweza kuzijaribu kwenye simu yako ya Android.
Kumbuka kuna list nyingine zaidi ya 20 ya app nzuri hivyo kama utaona app hizi sio nzuri kwako unaweza kutembelea hapa kwaajili ya kujua app nyingine nzuri za kujaribu kwenye simu yako ya Android. Basi baada ya kusema hayo twende tukaangalie apps nzuri kwa siku hii ya leo.
TABLE OF CONTENTS
insFull
InsFull ni appa nyingine nzuri sana ya Android kwaajili ya mtandao wa Instagram, App hii inakupa uwezo wa kuangalia profile picha ya mtu yoyote kwa haraka. App hii inauwezo wa kuonyesha picha hiyo kwa ukubwa kama picha nyingine kwenye mtandao huo wa Instagram.
Around Sound
Around Sound ni app nzuri sana ya kurekodi sauti, najua kuwa asilimia kubwa ya simu zinakuja na uwezo wa kurekodi sauti lakini app hii inakuja na uwezo wa tofauti kidogo. App hii inakupa uwezo wa ku-editi sauti baada ya kurekodi ikiwa pamoja na uwezo wa kuhifadhi sauti hizo kwenye Internet kwaajili ya kutunza ili uweze kuzipata pale unapo poteza simu au kubadilisha simu.
Discover
Discover ni app nyingine nzuri sana ambayo inakupa uwezo wa kubadilisha muonekano wa simu yako pale unapokuwa kwenye Lock Screen. App hii inakupa uwezo wa kuweka picha za vitu mbalimbali kwenye kioo chako pale simu yako inapokuwa imefunga. Unachotakiwa kufanya ni kuchagua category ya picha unazopenda kisha chagua picha kwa kupisha kidole kwenye kioo chako.
Typing Hero
Kama umekuwa ukipata shida ya kuandika maneno ya aina moja mara kwa mara basi lazima utaipenda app hii, App hii inakupa uwezo wa kuweka kifupi cha maneno na endapo ukiandika kifupi hicho wakati unaandika kitu chochote ndani ya simu yako basi neno zima litatokea. Kwa mfano umezoea kuandika neno Nitakucheki Kesho sasa kupitia app hii unaweza kuseti kila ukiandika herufi NK litokee neno Nitakucheki Kesho.
HQ Music
Kama wewe ni mpenzi wa kusikiliza muziki na upende kutumia muda mrefu kubonya simu yako kutafuta nyimbo fulani basi app hii itakufaa sana. App hii inakupa uwezo wa kusogeza nyimbo mbela na nyumba kwa kupitisha kidole chako kwenye kioo cha simu yako. Unaweza kupapasa kidole chako kwa kwenda chini kama unataka kurudisha nyimbo nyuma na pia juu kama unataka kupeleka mbele. Pia unaweza kuchagua sehemu nyingi za kushoto au kulia.
Story Saver
Story Saver ni app nyingine inayokupa uwezo wa kutumia mtandao wa instagram kwa urahisi, App hii inakupa uwezo wa kudownload picha na video za Stories ambazo mara nyingi hizi huwa ni vigumu sana kuweza kuzipata.
Touch Bar
Kama unatumia simu yako mara kwa mara na ungependa kutumia simu yako kwa haraka zaidi basi app hii ni nzuri sana kwako. Kupitia app hii utaweza kuongeza Menu mpya chini ya kioo cha simu yako ambapo utaweza kuweka vitu mbalimbali kama WhatsApp, Instagram au programu zingine ambazo unapenda kuzitumia mara kwa mara. App hii ni nzuri sana hasa kama unatumia simu yako kwa mkono mmoja kwa muda mrefu.
Over
Kama wewe unatumia app ya Instagram na ungependa kutengeneza Post nzuri zinazo vutia basi unahitaji app hii. App hii inakupa uwezo wa kutengeneza picha za mtindo mbalimbali iwe Stories au Post za kawaida app hii itakusaidia sana. Kingine kizuri ni kuwa app hii inakupa Template za kutumia hivyo unaweza kutengeneza picha kwa urahisi sana na kwa haraka.
Spotytube
Kama wewe ni mpenzi wa miziki mipya basi app hii ni nzuri sana kwako, App hii inakupa uwezo wa kusikiliza nyimbo mpya kwa urahisi ambazo nyimbo hizi zinakuwa kwenye mpangilio rahisi. Kwa mfano unaweza kupata list ya nyimbo bora kupitia mtandao wa Spotify pamoja na list nyingine mbalimbali. Nakushauri kupakua app hii kama wewe ni mpenzi wa muziki.
Na hizo ndio apps nzuri ambazo nimekuandalia kwa siku ya leo, kama umependa app hizi nzuri basi unaweza kuangalia app nyingine nzuri hapa, pia hakikisha unadownload app yetu ya Tanzania Tech kwaajili ya kupata habari zote mpya za Teknolojia kwa haraka zaidi.
Aisee hii apps inaenda slowly sana kwann
Kivipi..?