Hizi Hapa App Nzuri za Android Ambazo Hazipatikani Play Store

Download app hizi nzuri ambazo haziko kwenye soko la Play Store
app ambazo hazipo play store app ambazo hazipo play store

Android ni moja ya mfumo wa simu ambao unatumiwa na watu wengi sana kwa sasa, pamoja na kuwa mfumo unaotumiwa sana pia wapo wabunifu wengi sana wanao tengeneza programu kwaajili ya Android programu ambazo nyingi zinapatikana kwenye soko la Play Store na nyingine nyingi zinakuwa hazipatikana kutokana na kutokidhi vigezo na masharti kadhaa ya soko la Play Store.

Japokuwa app hizo hazijakidhi baadhi ya vigezo na masharti ya Play Store sio kwamba hazifai kwa matumizi lah.. bali app hizi nyingi huwa ni nzuri na zinaweza kukusaidia sana kurahisha matumizi kwenye simu yako ya Android ya kila siku. Sasa tofauti na Apple, android inakuja na mfumo mzuri ambao unaweza kuinstall programu bila kupitia kwenye soko la Play Store hivyo basi kutokana na hilo leo tutaweza kuangalia programu nzuri ambazo hazipo Play Store ikiwa pamoja na link ambapo unaweza kudownload app hizo kwa kupitia mfumo wa APK kwaajili ya kuinstall kwenye simu yako.

Advertisement

Basi bila kupoteza muda natumaini uko tayari na kama bado hakikisha unakuwa tayari kwani na uhakika utapenda app hizi nzuri za Android.

1. NewPipe

NewPipe hii ni app nzuri sana ya Android kwaajili ya wapenzi wa kuangalia video na kusikiliza muziki, App hii ni app kama ya YouTube ambayo inakupa uwezo wa zaidi ya YouTube kwa kukupa uwezo wa kudownload video, audio pamoja na kusikiliza video huku unafanya mambo mengine kwenye simu yako. Unaweza kupakua app hiyo kwa kutumia link hapo chini.

DOWNLOAD NEWPIPE

2. iRoot

Kwa wale wanaopenda kuroot simu zao iRoot ni moja kati ya App nzuri sana ambazo zinasaidia kuroot simu za aina mbalimbali. App hii haipatikani kwenye soko la Play Store lakini ni moja kati ya app ambayo inafanya kazi kweli. Unaweza kupakua app ya iRoot kwa kubofya link hapo chini.

DOWNLOAD iROOT

3. Stop AD

StopAd ni moja kati ya app nzuri sana ya kuondoa matangazo kwenye programu mbalimbali, app hii inauwezo wa kuondoa matangazo kwenye app pamoja na kuondoa matangazo kwenye vivinjari vya aina mbalimbali kama vile Google chrome pamoja na FireFox. Unaweza kudownload StopAd kwa kutumia link hapo chini.

DOWNLOAD STOPAD

4. ShowBox

Kama wewe ni mfuatilia wa tovuti ya Tanzania Tech basi lazima utakuwa unajua kuhusu app hii, app hii ni nzuri sana kwa wapenzi wa filamu pamoja na Series, unaweza kuangalia au kupakua movie mpya kabisa kwa kutumia app hii mbali ya hayo unaweza pia kupata habari mbalimbali za filamu kupitia app hii ya ShowBox. Unaweza kupakua app hii kwa kutumia link hapo chini.

DOWNLOAD SHOWBOX

5. XTune

Kama wewe ni mmoja wa watu wanaopenda kupakua nyimbo mbalimbali basi app ya Xtune ni nzuri sana kwako. Kwa kutumia app hii unaweza kupakua nyimbo mbalimbali kwa haraka kwa kutumia simu yako ya Android, unaweza kutumia app hii kudownload album au nyimbo za kawaida moja kwa moja kwa kutumia app hii. Unaweza kupakua app ya Xtune kupitia link hapo chini.

DOWNLOAD XTUNE

6. Mobdro

Mobdro ni app nyingine nzuri sana ambayo inakupa uwezo wa kuangalia TV moja kwa moja kwa kutumia simu yako ya Android, app hii inakupa uwezo wa kuangalia channel za nje za kulipia mabazo mara nyingi unazipata kwa kulipia kingamuzi kama DSTV au Azam. Download app ya Mobdro kwa kutumia link hapo chini.

DOWNLOAD MOBDRO

Na hizo ndio baadhi tu ya app ambazo huwezi kuzipata kupitia soko la Play Store lakini ni App nzuri sana. Kama unataka kujua app nyingine nzuri za Android hakikisha unasoma makala yetu iliyopita ya app nzuri.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use