Katika ulimwengu huu wa teknolojia ni wazi kuwa kutumia Artificial intelligence au (AI) hakuepukiki hasa kama wewe unategemea simu yako kufanya mambo mbalimbali.
Kuliona hili leo nime kuletea apps nzuri za AI muhimu kuwa nazo kwenye simu yako wewe mtumiaji wa Android au iOS. Binafsi natumia apps hizi kila siku kufanya mambo mbalimbali na zimekuwa zikinisaidia sana kufanya mambo kwa urahisi. Basi bila kupoteza muda twende kwenye apps hizi.
TABLE OF CONTENTS
ChatGPT By OpenAI
Kama mpaka sasa huna app ya ChatGPT kwenye simu yako basi ni wazi kuwa utakuwa unakosa mambo mengi sana, mbali ya kuwa app hii imekuwa ikinisaidia kurahisisha mambo lakini pia nimekuwa nikitumia kurahisisha baadhi ya kazi zangu binafsi.
Kwa kulipa kiasi cha $20 sawa na takribani TZS 50,000 nimekuwa nikitumia app hii kufanya research, kuandaa makala na mambo mengi ya muhimu ambayo pengine ninge tumia muda mwingi sana bila kutumia app hii. Nakushauri pakua app hii kwenye simu yako na itumie utakuja kunishukuru.
Claude by Anthropic
App nyingine ambayo ni bora sana kuwa nayo kwenye simu yako hasa kama wewe unafanya research, au wewe ni developer au hata kama wewe ni mwanafunzi app hii ni muhimu sana kuwa nayo kwenye simu yako.
Kama ilivyo chatGPT Claude ni app ambayo inafanya kazi sawa na ChatGPT lakini hii inakuja na utofauti kidogo kwani haina uwezo wa kutumia Internet lakini inauwezo wa kujibu maswali mengi kwa wakati mmoja kuliko ChatGPT. Kama wewe ni developer utaona Claude inauwezo wa kutatua matatizo kwa urahisi zaidi kuliko ChatGPT, mbali na hayo app zote mbili zinafanana kwa matumizi.
Perplexity AI
Kama kwa muda umekuwa ukitumia Google pekee kupata majibu ya maswali yako mtandaoni basi pengine ni vyema kutafuta njia nyingine kwani Google imekuwa ikibadilika kila siku na pengine kuna baadhi ya maswali Google haipo vizuri sana kujibu maswali yako.
Ndio maana nimekuletea app hii ya Perplexity AI, app hii itakusaidia kujibu maswali yako kwa kutumia AI kwa urahisi bila kubofya link mbalimbali. Utaweza kupata majibu kwa urahisi zaidi na kama unataka kujua zaidi unaweza kubofya link, lakini app hii inaweza kukupa majibu kwa haraka zaidi bila kwenda kwenye tovuti yoyote.
Gemini By Google
Kama wewe ni mmoja watumiaji wa huduma za Google “nani ambae sio mtumiaji” app hii ni muhimu sana kuwa nayo kwenye simu yako. Google Gemini AI ni mfumo wa akili badindia wa Google ambao hivi karibuni umeboreshwa zaidi.
Kama unatumia huduma kama YouTube, Google Map, Google Doc na huduma nyingine nyingi za Google app hii ni muhimu kwani inasaidia kupata msaada kutoka kwenye huduma za Google kwa urahisi. App ya Gemini imeanza kupatikana hivi karibuni na unaweza kuinstall kwenye simu yako na kuuliza maswali kama ilivyo kwenye app nyingine zilizopita hapo juu.
Kwa watumiaji wa Android unaweza kupakua app ya Gemini moja kwa moja lakini kwa watumiaji wa iOS utaweza kutumia Gemini AI kupitia app ya Google.
Microsoft Copilot
Microsoft Copilot ni app nyingine ambayo ni bora kuwa nayo kwenye simu yako, app hii haina tofauti sana Google Gemini na inakupa uwezo wa kupata majibu ya maswali yako kwa urahisi kupitia Bing Search.
Mbali na hayo mfumo wa Microsoft Copilot unatumia teknolojia ya OpenAI hivyo baadhi ya majibu ambayo ungepata kupitia mfumo wa ChatGPT.
Na hizi ndio apps muhimu kuwa nazo kwenye simu yako kama wewe ni mmoja wa watu wanao tumia simu yako kufanya mambo mbalimbali. Kama unataka kujua apps nyingine nzuri za kuwa nazo kwenye simu yako basi hakikisha unapitia tovuti ya Tanzania Tech kila siku.
Kwa urahisi zaidi hakikisha unapakua app ya Tanzania Tech na kubadilisha lugha kwenda Kiswahili.
Ili kubadilisha lugha bofya kitufe cha menu upande wa kulia juu kisha bofya “Swahili Site” kisha bofya “Choose” alafu chagua “Kiswahili” kisha maliza kwa kubofya “Save”.
Baada ya hapo funga app ya Tanzania Tech na fungua na utakuwa unasoma makala za Kiswahili na huna haja ya kubadilisha lugha tena kama unataka kuendelea kupata makala za Kiswahili.