Umepita muda mrefu kidogo toka tujadili kuhusu app nzuri za kujaribu kwenye simu yako ya Android, lakini leo nimeona nikuletee list ya app hizi chache ambazo naamini zinaweza kusaidia kufanya mambo mbalimbali kwa urahisi kwenye simu yako ya Android.
Basi bila kuendelea kupoteza muda zaidi basi moja kwa moja twende kwenye list hii, kumbuka kuwa unaweza kupakua app zilizo tajwa kwenye list hii kwa kubofya jina la app husika.
TABLE OF CONTENTS
FilmPlus
Kama wewe ni mpenzi wa movie na ungependa kudownload Movie moja kwa moja kupitia simu yako ya mkononi ya Android basi app ya FilmPlus ni app bora sana kwako, kupitia app hii utaweza kudownload movie zote mpya kwa urahisi na haraka, app hii ni rahisi kutumia na utapata movie yoyote ile unayotaka ikiwa pamoja na series mpya.
Notepin
Notepin ni app nzuri sana ambayo itakusaidia kuweza kukumbuka mambo mbalimbali kwa urahisi na haraka, app hii inakupa nafasi ya kuweza kutengeneza Notes na kuziweka kwenye sehemu ya juu ya notification kwenye simu yako na kila unapfungua sehemu hiyo utaweza kuona Notes hizo na hivyo kukumbuka ulichokuwa unataka kufanya.
Assistive Touch
Assistive Touch ni app nyingine nzuri ambayo itakusaidia kufanya mambo kwa haraka kwenye simu yako ya Android. App hii inakuja na shortcut kama ile inayo patikana kwenye iPhone ambayo itakusaidia kufanya mambo kwa haraka kama vile kuwasha tochi, kufungua app mbalimbali na mambo mengine mbalimbali.
Walldrobe
Kama unapenda kubadilisha muonekano wa simu yako kwa kutumia wallpaper basi app hii ni nzuri sana kwako. App hii inakuja na mkusanyiko wa wallpaper mbalimbali ambazo unaweza kutumia kwenye simu yako ya Android kwa haraka na urahisi.
24/7 Voice Recorder
Kama wewe ni mtu ambaye unapenda kuweka kumbukumbu ya siku yako nzima jinsi ilivyokuwa basi jaribu app hii ya 24/7 Voice Recorder. App hii inakupa nafasi ya kurekodi kwa masaa 24 yaani siku nzima huku ikigawanyisha rekodi hizo kwa masaa. App hii ni nzuri kama unataka kuweka kumbumbu ya vitu vyako binafsi ambavyo umekuwa ukifanya kila siku.
SHEROES
App nyingine kwenye list hii inahusu sana wanawake, app hii ni mtandao wa kijamii ambao ni maalum kwaajii ya wanawake. App hii inaonekana kupendwa na watu wengi sana. Kama wewe ni mwanamke basi unaweza kujaribu mtandao mpya wa kijamii kwa ajili yako.
Ad Maker
Ni wazi kuwa kwa sasa hakuna biashara inaweza kwenda bila kufanya matangazo na kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanataka kitengeneza tangazo bora ambalo unaweza kulitumia kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram na mitandao mingine basi app hii ya Ad Maker ni app bora sana kwako. App hii inakupa uwezo wa kutengeneza matangazo kwa urahisi na haraka kwa kutumia simu yako ya Android.
Gazeti Lite
Gazeti Lite ni app itakayokupa uwezo wa kusoma Magazeti ya leo pamoja na habari mbalimbali kwa urahisi kutoka tovuti mbalimbali bila kutumia Internet, Mbali ya kuwa unaweza kusoma habari kupitia tovuti mbalimbali pia utaweza kupata habari kutoka akaunti za mitandao ya kijamii kama Instagram na Facebook. Pia utaweza kuchangia mada na mijadala mbalimbali kutoka Jamii Forums.
Tanzania Tech
Kama unataka kupata habari zote hizi kupitia simu yako ya mkononi basi app ya Tanzania tech. App hii ni rahisi kutumia na unaweza kupata habari zote za teknolojia kutoka Tanzania Tech kwa urahisi na haraka.
Na hizo ndio apps nzuri nilizo kuandalia kwa siku ya leo. Kama unataka kujua apps nyingine nzuri, unaweza kusoma hapa kujua apps nzuri zitakazo kusaidia kuangalia mpira kupitia simu yako ya mkononi.
Habari tanzania tech, kwasasa naona gazeti lite app haipatikani play store kwahiyo naomba link yake,asante.
Tumesha kujibu kupitia barua pepe.
Nimependa hii sana ongera sana