Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mfumo wa Android Sasa Ndio Unaongoza kwa Kutumiwa Sana

Android yapita windows, sasa ndio mfumo unaotumiwa sana duniani
Mfumo wa Android Sasa Ndio Unaongoza kwa Kutumiwa Sana Mfumo wa Android Sasa Ndio Unaongoza kwa Kutumiwa Sana

Kwa sasa simu ni moja kati ya vitu muhimu sana kuliko hata kompyuta zetu, tumekua tukitumia simu kwa muda mwingi sana kuliko hata tunavyotumia kompyuta ndio maana hadi mwezi march 2017 ripoti zinaonyesha mfumo wa Android ni mfumo unaotumika sana duniani kuliko mfumo wa Windows ambao ndio ulikua ukiongoza hapo mwaka jana 2016.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka kampuni ya utafiti ya StatCounter, ripoti hizo zinasema kuwa watumiaji asilimia 37.98 kwa sasa wanatumia Android huku watumiaji wa Windows wakiwa ni asilimia 37.91 kati ya watu wote ambao walifanyiwa utafiti na kampuni hiyo. Hata hivyo Kampuni hiyo ilifanikiwa kufanya tafiti hiyo kwa kutumia zaidi ya tovuti milioni 2.5 ambazo zinawatumiaji zaidi ya bilioni 15 kwa mwezi huku ikiangalia matumizi ya mifumo ya uendeshaji ya vifaa mbalimbali ya Android, Windows, iOS pamoja na OS X au (MacOS).

Advertisement

Kwa upande wa mifumo ya iOS na MacOS mabadiliko makubwa yako kwa upande wa iOS kwani watumiaji wake wamekua ni wengi mara tatu zaidi kuliko wale wa MacOS hii ikiwa na maana ya kuwa watumiaji wa simu zenye mfumo wa iOS ni wengi kuliko watumiaji wa kompyuta za MacOS au iOSX.

Ripoti hii inaonyesha mabadiliko makubwa pamoja na ongezeko kubwa la watumiaji wa simu za mkononi huku simu zenye kutumia mfumo ya Android zikionekana kutawala hata matumizi ya kompyuta. Niwakati sasa wa kampuni pamoja na watu mbalimbali kutengeneza teknolojia zenye uwezo wa kufanya kazi kwenye simu kwani kwa sasa ndipo ulimwengu unapo elekea.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use