Ni wazi kuwa kuandika ni kazi ngumu sana, haijalishi una andika kwa mkono au una andika kwa kutumia kompyuta. Kuliona hili leo nimekuletea makala ambayo itakusaidia kurahisha kazi ya kuandika hasa kama unataka kuandika kwa kutumia lugha ya kingereza.
Kupitia makala hii utaweza kujifunza njia rahisi ya kuandika kwa kutumia mfumo wa AI au Artificial intelligence ambapo utaweza kuandika kwa lugha ya kiingereza kwa urahisi. Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye makala hii.
Kwa kuanza ni muhimu kujua kuwa njia hii inafanya kazi kama unataka kuandika kwa lugha ya Kiingereza na sio Kiswahili.
Kwa kuanza moja kwa moja download app kupitia link hapo chini, hakikisha una install app hii vizuri kwenye simu yako.
Baada ya kudownload fungua app hii ni moja kwa moja utaona list ya vitu ambavyo mfumo wa AI au app hii inaweza kufanya, unaweza kuchagua kitu ambacho unataka kufanya kwa mfano kuandika barua pepe au blog post.
Baada ya kuchagua kitu unachotaka kufanya, moja kwa moja utaona ume letewa box la kuandika, kwenye box hilo andika kichwa cha habari tu, hakikisha maneno hayo yanakua kwenye lugha ya Kiingereza kisha baada ya hapo bofya Generate.
Baada ya kubofya Generate hakikisha una internet kwenye simu yako kisha subiria ndani ya sekunde chache na moja kwa moja utaweza kuona barua pepe nzima ikiwa imeandikwa kulingana na kichwa cha habari ambacho umeandika hapo awali.
Kama unavyoweza kuona hapo juu, baada ya kuandika kichwa cha habari “Request for comments” moja kwa moja app hii imeweza kutengeneza email ambayo inahusiana na kichwa cha habari hicho na moja kwa moja unaweza kucopy email hiyo na kuedit unavyotaka.
Unaweza kufanya zaidi ya kuandika email, unaweza kufanya mambo mengi kama unavyoweza kuona kwenye picha ya kwanza kabisa hapo juu. Kitu cha muhimu hakikisha una andika maneno machache kuhusu unachotaka na moja kwa moja app hii itaweza kuandika chochote kwa sekunde chache
Na hiyo ndio njia rahisi ambayo unaweza kutumia kuandika kwa kutumia AI au Artificial intelligence. Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kuedit PDF kupitia simu, au kama unataka kuedit kwa kutumia kompyuta unaweza kusoma hapa.