Hivi karibuni kampuni ya Amazon kupitia tovuti yake ya amazon.com imeanza kufanya majaribio ya kuja na programu yake mpya ya kuchat inayoitwa Anytime, imeripoti tovuti ya The verge. Hata hivyo inasemekana kuwa kampuni hiyo kwa sasa inafanya utafiti mbalimbali kuhusu sehemu za programu hiyo na bado haijajulikana programu hiyo ikimalizika itakuja na sehemu gani.
Hata hivyo taarifa zingine zilizotolewa na tovuti ya habari ya aftvnews zinasema kuwa programu hiyo itakuwa na sehemu mbalimbali kama vile sehemu ya kuchat kwa meseji, sehemu ya kupiga simu za sauti na vilevile sehemu ya kutuma picha pamoja na sehemu ya kuweka urembo mbalimbali kwenye picha maarufu kama filters.
Sehemu nyingine ambazo zimeripotiwa na tovuti hiyo ni kama @mention, kutumia sticker, kutumia Gifs, pamoja na kucheza games mbalimbali kupitia app au programu hiyo. Tovuti hiyo inaendelea kusema kuwa, watumiaji wataweza kuchat na magroup mbalimbali au mtu mmoja mmoja huku app hiyo ikiwa na uwezo wa kusaidia kununua bidhaa kupitia tovuti maarufu ya amazon.com.
Vilevile kwa mujibu wa tovuti ya theverge programu hiyo itakuja ikiwa na uwezo wa kutumika kwenye simu za mkononi maarufu kama smartphone na hata pia kwenye kompyuta mbalimbali, lakini zaidi ni kuwa programu hiyo pia itakuja na ulinzi wa hali ya juu sana huku mazungumzo ya watumiaji wa app hiyo yakiwa encrypted ili kuzuia mtu asiweze kudukua na kusoma meseji baina ya watumiaji.
Amazon tayari ilisha anza kutengeneza programu mbalimbali za kushindana na Facebook pamoja na WhatsApp kwa kutengeneza programu ya Chime hapo mwaka jana, programu hiyo ilitengenezwa kwaajili ya kusaidia wateja wake wa bidhaa kupitia tovuti ya amazon.com. Hata hivyo bado mpaka sasa amazon haijasibitisha habari hizi za kuja na programu mpya ila tutakuletea muendelezo wa habari hii pindi tutakapo pata habari zaidi.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.