Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Fahamu Amazon Go Duka la Kwanza la Kielektroniki Lisilo na Muuzaji

Je unaweza kuiba kwenye duka hili..? Soma kujua zaidi
Duka la Amazon Go Duka la Amazon Go

Hivi karibuni, kampuni ya Amazon imefungua duka lake la kilektroniki lisilo kuwa na muuzaji la Amazon Go, duka hili ni la kwanza duniani kutumia teknolojia ya AI au Artificial Intelligence na kwa sasa lime funguliwa rasmi huko nchini marekani na leo tutaenda kuangalia jinsi duka hilo linavyo fanya kazi.

Duka hili lime tengenezwa kwa teknolojia ya kisasa huku liki saidiwa na watu mbalimbali pamoja na kamera za ulinzi kwa ajili ya kufanya huduma za duka hilo kuwa rahisi. Lakini pengine una jiuliza mtu ana wezaje kulipia pesa anapo nunua kitu na wakati duka hilo halina muuzaji. Basi labda nikueleze kidogo, hapa amazon inatumia programu maalum ambayo ni lazima kuwa nayo kwenye simu (smartphone) yako kabla ya kuingia kwenye duka hilo.

Advertisement

Wakati unaingia kwenye duka hilo, utawasha programu hiyo kisha utaweka simu yako juu ya kioo maalum ambacho kitasoma data zako maalum ambazo utakua ulijaza wakati wa kujisajili na app hiyo pamoja na mtandao wa Amazon kwa ujumla. Pia ni lazima uwe ni mwanachama au umejisajili na mtandao wa Amazon ikiwa pamoja na kuweka kadi yako ya bank kwa ajili ya manunuzi mbalimbali.

Ukisha ingia kwenye duka hilo la Amazon Go kutakuwa na mtu wa kukagua kitambulisho chako kisha uta ruhusiwa kuanza kufanya manunuzi au kuchukua kitu chochote unachotaka ndani ya duka hilo bila uangalizi wa mtu yoyote.

Lakini hautokuwa mwenye kabisa bali hapa kamera mbalimbali za ulinzi kwa kushirikiana na sensor maalum ndio zitakuwa zinatambua ni kitu gani umechukua kutokana na alama zilizo wekwa kwenye bidhaa. Sensor hizo ziko kila maahali ndani ya duka hilo ikiwa pamoja na kwenye mashelfu yaliyo na vitu pamoja na juu kwenye paa la duka hilo ambalo ni limetengezwa kwa vioo.

Baada ya kuchukua kila unachotaka utatoka moja kwa moja kwenye duka hilo na wakati umefika nje kidogo ya duka hilo basi utaletewa ujumbe maalum ambao utaonyesha orodha ya vitu vyote ambavyo umenunua ikiwa pamoja na gharama ulizo tumia kununua vitu hivyo. Lakini haija ishia hapo, kama unahisi umekatwa pesa kwa kitu ambacho huku chukua basi kwa kutumia app hiyo unaweza kutoa ripoti na pesa zako zitarudishwa kwenye akaunti yako ya bank.

Vilevile unaweza kurudisha bidhaa yoyote kwa kutumia App hiyo, lakini mpaka sasa inasemakana kwa kutumia njia hiyo watu wamekua wakiondoka na bidhaa bila kurudisha ndani ya duka hilo sababu hakuna mfumo wa kurudisha ndani ya duka hilo.

Lakini kila kizuri akikosi kasoro, ikiwa duka hilo lime funguliwa kwa muda wa wiki moja na nusu tu mpaka sasa, kumekua na ripoti za watu kufanikiwa kuiba vitu mbalimbali ingawa kampuni ya Amazon inasema ni ngumu kwa mtu kuweza kufanya hivyo.

Sasa watu wengi wameripoti kwenye mitandao mbalimbali kuwa unaweza kuiba kwenye duka hilo japokuwa kampuni hiyo bado inasema kuwa jambo hilo hali wezekani, hapa sita kuchosha na maneno mengi angalia video hapo chini.

Tuambie nini maoni yako kuhusu duka hili, unadhani hii ni teknolojia itakayoweza kuja Tanzania au Afrika kwa ujumla. Tumabie kwenye maoni hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

1 comments
  1. Nimependa sana app hii maana mimi ni mdao wa vifaa vya umeme mf.kompyuta, printa n.k hivyo naamini kuwa nitanufaika sana na app hii.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use