Ni wazi kuwa lazima utakuwa umewahi kusikia neno “Always On”, kama hujawahi kusikia neno hilo basi kupitia makala hii nitaenda kukufahamisha kuhusu teknolojia hii, ikiwa pamoja na jinsi ya kuipata teknolojia hii kwenye simu yako ya Android.
TABLE OF CONTENTS
Always On ni nini.?
Kwa kuanza labda ufahamu kuhusu teknolojia hii ya Always on. Always on ni sehemu ambayo inapatikana zaidi kwenye simu za Android, sehemu hii huweza kufanya simu yako kuweza kuonyesha data mbalimbali wakati simu yako ikiwa imelala au kioo cha simu kikiwa kime zimwa.
Always on huonyesha data mbalimbali kama vile missed calls, kalenda, muda pamoja na taarifa nyingine mbalimbali kama WhatsApp meseji, Barua pepe na taarifa nyingine mbalimbali za simu.
Mara nyingi always on inapatikana kwenye simu nyingi za Android ambazo zinatumia mfumo wa kuanzia Android 9 na kuendelea, sehemu hii inapatikana kupitia Settings > Display kisha tafuta always on. Kama simu yako haijawezeshwa na always on, maana yake ni kuwa huwezi kutumia sehemu hiyo moja kwa moja kupitia settings. Lakini zipo njia za kupata yoyote ya Android.
Always On Kwenye Simu Yoyote
Kama simu yako haina sehemu ya Always on kupitia sehemu ya Setting > Display kwenye simu yako, basi moja kwa moja unaweza kutumia njia hii ili kuweka Always on kwenye simu yako. Kitu cha muhimu hakikisha unatumia simu ya Android yenye mfumo wa Android kuanzia Android 5 na kuendelea.
Kwa kuanza unatakiwa kupakua app ya Always on kupitia link hapo chini, app pia inapatikana Play Store lakini zipo app nyingi za mtindo huu ambazo zinapatikana play store lakini tatizo kubwa ni kuwa app hizo zinakuja na matangazo mengi sana. App kwenye link hapo chini haina matangazo kabisa hivyo hutopata tatizo lolote la kusumbuliwa na matangazo wakati wa kutumia.
Download App ya Always On Hapa
Baada ya kudownload app hiyo install kwenye simu yako kisha fuata maelekezo haya kwenye app hiyo, baada ya kumaliza kufanya kila kitu kinacho elekezwa kwenye app hiyo utaweza sasa kuona kioo cha always on kikiwa kina onyesha notification mbalimbali, ikiwa pamoja na saa na tarehe.
Mpaka hapo natumani utakuwa umeweza kuwasha Always on kwenye simu yako yoyote ya Android, kama unataka kujifunza zaidi, unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kufungua programu yoyote kwa haraka kwa kupiga piga mara mbili nyuma ya simu yako. Kwa maujanja kwa vitendo hakikisha una subscribe kwenye channel Yetu ya Tanzania Tech hapa.